Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewapiga marufuku wanasiasa
ambao wanaeneza maneno ya uchochezi katika mkoa wake na kuwataka
wananchi wawapuuze.
Makonda
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa anakabidhi magari 10
kwa kampuni ya DAR COACH kwa ajili ya matengenezo ambayo yatakamilika
kwa muda wa siku 110 huku gharama yake ikiwa ni zaidi ya bilioni 1.
RC
Makonda ameeleza kuwa wanasiasa wa namna hiyo hawahitaji katika Mkoa
wake, vinginevyo ni vyema washirikiane kuijenga Dar es Salaam mpya.
"
Kauli za kebehi, kutukanisha, kufarakanisha na kuchonganisha
hazitusaidii katika ujenzi wa Dar es Salaam mpya, hivyo ni waombe na
ninafikiri wanafahamu mimi siyo muoga na katika watu wanaojiamini katika
Mkoa huu ni mimi hapa, kwenye nchi atabaki Rais, na katika wakuu wa
Mikoa wanao jiamini mimi najitosha, nisinge penda tujaribiana na
kuchafuliana miji, kama unataka kutoka kauli ya uchochezi katolee kwenye
Mkoa wako, na nimepata taarifa mmoja mnae kaeni nae ". Alisema RC
Makonda.
RC
Makonda ameshangaa kuona wanaosema serikali imepoteza dira huku akisema
serikali ya awamu ya tano imefanya makubwa ikiwemo suala la Rais
kuidhinisha fedha za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, elimu bure kwa
wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, kulipwa kwa deni la zaidi ya
trilioni 1 ambalo serilai ilikuwa inadaiwa na taasisi mbalimbali
"
Unasema dira hakuna wakati wanafunzi walikuwa wanalipa ada, wakati huu
hawalipi, unasemahuoni dira wakati wanafunzi walikuwa wanagoma kwa
kukosa mikopo Rais anaidhinisha unasema huoni dira, nchi ilikuwa haina
ndege serikali imeleta ndege unasema huoni dira, reli ya starndard gauge
inajengwa gharama za serkali unasema huoni dira, kweli kuna haja ya
kuwa na hospitali ya milembe kwenye kila mkoa" Alisema RC Makonda.
Siku
ya jana aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu,
alijiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na nyadhiza zake
zote za ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai serikali
ya awamu ya tano imepoteza dira jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda analipiga marufuku.
Vilevile
siku ya leo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa kutoa maneno ya uchochezi katika ufunguzi wa kampeni
za udiwani kata ya Kijichi wilaya ya Temeke, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa
amepiga marufuku kwa mwanasiasa yeyote kufanya uchochezi badala ya
kuhamasisha maendeleo.
No comments:
Post a Comment