Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisiitiza jambo wakati
wa ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya
kuvuna lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu Kikuu cha Dar
es salaam leo Novemba 8, 2017.
Wadau
wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna wakifatilia Kongamano
lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo Kikuu cha Dar es salaam Leo
Novemba 8, 2017.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada
ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma,
Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.
Baadhi
ya washiriki wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada
ya kuvuna wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma,
Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.
Washiriki
wa Kongamano la wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya kuvuna
wakifatilia Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkuruma, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam leo Novemba 8, 2017.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Novemba 8, 2017
amefungua Kongamano la Wadau wa Mazao ya Chakula wakati na baada ya
kuvuna lenye dhima ya kujadili masuala muhimu yanayohusiana na PHM na
mchango wake katika uhakika wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa
viwanda nchini Tanzania kwa ajili ya kupunguza upotevu, kuimarisha
usalama wa chakula na kuchochea uanzishwaji wa viwanda.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika Katika Ukumbi wa
Chuo Kikuu cha Dar es salaam Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa alisema kuwa
anataraji kongamano hilo litakuwa na mjadala muhimu kujadili masuala
muhimu yanayohusiana na Kuzuia Upotevu wa Mazao kabla na baada ya
kuvunwa (PHM).
Alisema
Serikali imeweka msisitizo wa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi
na kwa Wabia wa Maendeleo kuwekeza katika eneo hilo la PHM.
“Serikali
kwa kuzingatia umuhimu wa sekta binafsi itahakikisha mchakato wa
kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza upotevu unakuwa shirikishi na
unatekelezwa na wadau kwa ufanisi”
“Nadhani
mtakubaliana na mimi kuwa hili ni tukio kubwa sana kwa Wadau wa Mpango
wa kupunguza Upotevu wa Mazao baada ya Kuvunwa (PHM) nchini tangu
jitihada za kushughulikia suala hili zianze na kwa sasa suala hili
linaanza kueleweka kwa wadau wengi tofauti na uko nyuma ambako msisitizo
ulikuwa juu ya uzalishaji na tija” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema,
Kulingana na takwimu zilizopo bado kuna upotevu mkubwa wa mazao ya
chakula ambao unafikia wastani wa asilimia 30 mpaka 40 kwa mazao ya
nafaka na mikunde na kwa wastani wa asilimia 50 kwa mazao ya mboga na
matunda.
Alisema
ili kupunguza upotevu wa mazao ni muhimu sana na ni mkakati mzuri wa
kuihakikishia nchi usalama wa chakula na lishe. Kuwepo kwa chakula cha
kutosha katika Taifa na katika ngazi ya kaya ni msingi wa Taifa lenye
uchumi imara, watu wenye afya nzuri na amani. Alisema kuwa jitihada za
kushughulikia UPOTEVU WA MAZAO BAADA YA KUVUNWA zilianza miaka ya 1980
baada ya kujitokeza kwa wadudu waharibifu wa mazao wajulikanao kama
Dumuzi ambao walisababisha upotevu mkubwa wa mazao na kuhatarisha
uhakika wa chakula nchini Tanzania.
Aliongeza
kuwa Kuanzia wakati huo mabadiliko ya kisera katika sekta ya kilimo
yalianza kujitokeza kupitia Serikali ya Tanzania hasa madiliko
yanayolenga kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvunwa. Sambamba na
hayo pia alisema kuwa jitihada nyingi nchini Tanzania za kupunguza
upotevu wa mazao zimefanyika zikiwemo Kujenga maghala kupitia Miradi
mbalimbali, Kuanzishwa Kitengo cha Hifadhi na Usindikaji wa Mazao, chini
ya Idara ya Usalama wa Chakula na jukwaa la wadau (TPMP), Kuanzishwa
kwa mashirika ya kubuni teknolojia mbali mbali zinazohusiana na PHM kama
vile SIDO, CAMARTEC, Kuigizwa kwa masuala ya PHM kwenye Programu ya
Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), na Kuanzishwa kwa miradi na juhudi
mbalimbali zinazohusu PHM kama vile MIVARF, GPLP, COWABAMA.
Mhe
Mwanjelwa alibainisha kuwa jitihada zote hizo hazikufanikiwa vizuri kwa
sababu ya kukosa mfumo mzuri wa kuratibu kazi zote PHM zilizotekelezwa
na wadau mbalimbali matokeo yake kukajitokeza wadau kutekeleza kazi
zinazofanana bila kujuana na maeneo mengine hayakushughulikiwa
kikamilifu. Hali hii ili sababisha matumizi mabaya ya rasilima na
kushindwa kuwa na mipango madhubuti ya kutekeleza shughuli za
maendeleo.
Aidha,
aliwataarifa kuwa maandalizi ya Mkakati wa Kuzuia Upotevu wa Taifa yako
hatua za mwisho ambapo Mkakati huo utaunganisha wadau wote
wanaojishughulisha na kazi za kupunguza au kuzuia upotevu wa mazao ya
chakula.
“Ni
Imani yangu kama mkakati huo utatekelezwa kikamilifu upotevu wa mazao
utapungua kufikia wastani wa asilimia 5 nchini Tanzania” Alisisitiza
Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa.
Ksatika
hatua nyingine Mhe Mwanjelwa alilipongeza jukwaa la wadau (TPMP) kwa
kushirikiana vizuri na Wizara ya Kilimo, HELVETAS, Swiss
Inter-cooperation-Tanzania, ANSAF na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
maandalizi ya kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment