Mwenyekiti
wa muda wa Wazazi Mburahati Saccos, John Mapunda akifungua mkutano wa
wanachama wa Saccos hiyo, uliofanyika kwenye ukumi wa Jengo la
Kitegauchumi la CCM, Mburahati, Dar es Salaam, jana. Amesema ameamua
yeye na wenzake kuanzisha ushirika huo wa Akiba na mikopo siyo kwa
maslahi ya kisiasa bali kuwasaidia kuwasaidia kiuchumi wanachama wa
Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Mburahati ili nao waweze kuwa na maisha
bora wakiwa ni miongoni mwa Watanzanaia wenye mahitaji hayo. Kushoto ni
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo ambaye alifika
kwenye mkutano huo kutoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha na kuendesha
Saccos. Kulia ni Mhazini wa muda Boniface Chigenda na Katibu wa muda
Sofia Kiroboto.
Ofisa
Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akitoa mafunzo ya namna
bora ya kuanzisha Saccos na kuifanya idumu wakati wa mkutano huo.
Amesema Saccos hiyo kwa sasa imeshatimiza masharti yote ya kupatiwa
usajili na inapatiwa usajili huo hivi karibuni, alisema katika Kadirio
lake Saccos hiyo inatarajia kupata zaidi ya Sh. milioni 13 kutokana na
ada na michango ya wanachama ambao hadi sasa wamefikia 68, pia kufanya
matumizi ya zaidi ya Sh. milioni 13 na kubaki na ziada ya zaidi ya Sh.
milioni 29.
Kitabu au Masharti ya Saccos hiyo
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo, akionyesha
orodha ya wananchama 68 waliokwishajiunga na Saccos hiyo. Kulia ni
Mwenyekiti wa muda John Mapunda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya
Wazazi Kata ya Mburahati.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akifafanua jambo wakati akionyesha orodha hiyo
Baadhi ya wanachama wa Saccos hiyo wakisikiliza Ofisa huyo kwa makini
Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo John Mapunda akitoa nafasi kwa wanachama kuuliza maswali

Mwanachama wa Saccos hiyo Dismas Shirima akiuliza swali.
Mwanachama wa Saccos hiyo Mtindi Mbega akiuliza swali
Ofisa
Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo (kushoto), akimsikiliza
kwa makini Mwanachama wa Saccos hiyo Justin Kaijage wakati akiluzwa
swali
Mwenyekiti
wa muda wa Saccos hiyo John Mapunda na Katibu wake Sofia Kiroboto
wakifuatilia kwa karibu wakati wanachama wakiuliza maswali
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akijibu maswali
wanachama ukumbini
Wanachama ukumbini
Wanachama ukumbini
Wanachama wakichangamkia kulipa ada
Wanachama wakichangamkia kulipa ada
Mtoto wa mmoja wa wanachama wa SACCOS akijiburudisha kwa soka wakati mkutano ukiendelea
Ofisa
Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo (kulia) akiagana na
wanachama waanzilishi wa Saccos hiyo, Dickson Tungaraza, baada ya kikao
kumalizika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment