Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla
(kushoto) mabati yaliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu
Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi
katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya
mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika
ndani ya Meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, nondo
zilizochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa
lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa
Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya
saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam
Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini
Pemba, Mwajuma Majid Abdalla.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuonyesha
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto), na Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, mifuko ya saruji
iliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa
lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa
Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya
saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam
Sealink katika Bandari ya Mkoani mara baada ya meli hiyo kuwasili na
mizigo hiyo kutoka jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
wananchi wa Pemba pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara
baada kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba za polisi katika
Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba, Zanzibar. Katika hotuba yake,
Masauni alisema wadau wamemchangia shilingi milioni 400 kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba 12 za Jeshi la Polisi ili kukabiliana na ukosefu wa
nyumba za polisi katika mikoa hiyo. Awamu ya ujenzi wa nyumba hizo ni ya
kwanza, na awamu ya pili itakua mikoa ya mipya nchini ambayo ni Geita,
Simiyu, Katavi na Songwe. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Mwajuma
Majid Abdalla, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia)
akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (wapili
kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman
(kulia), wakitoka ndani ya meli ya Azam Sealink katika bandari ya
Mkoani, mara baada ya Naibu Waziri Masauni kuwakabidhi mifuko ya saruji,
mabati, ndoo za rangi pamoja na nondo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa
nyumba za polisi katika mikoa hiyo ya Pemba.
Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Othman akimfafanulia jambo Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili
kushoto), katika kikao cha ndani kilichofanyika katika ukumbi wa Bandari
ya Mkoani, kabla ya Naibu Waziri Masauni hajawakabidhi vifaa vya ujenzi
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika mikoa ya
Pemba. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi, Ustawi wa Jamii,
Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Zanzibar, Shadia Mohamedi Suleiman,
wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, na
kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis
Haji.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea tunda
aina ya fenesi kutoka kwa Mkazi wa Chakechake Pemba, Kauthar Issihaka
mara baada ya Naibu Waziri huyo kukabidhi vifaa vya ujenzi wa nyumba 12
za polisi katika Mikoa ya Pemba. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika
katika Bandari ya Mkoani mara baada ya Meli ya Azam ya Sealink kufikisha
vifaa hivyo kutoka jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman na kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Kusini Pemba, Shahani Mohamed Shahani.
NAIBU
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
amewahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini na kufanikisha
kupata vifaa vya ujenzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa nyumba za Polisi
Mikoa ya Pemba, Zanzibar.
Mradi
huo umeanza katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo
nyumba kumi na mbili zinatarajiwa kujengwa ili kufanikisha askari na
Maafisa wa Jeshi la Polisi ndani ya mikoa hiyo waweze kuishi katika
nyumba za jeshi pamoja na kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za
makazi ya polisi hao, pia mradi huo utajenga nyumba katika mikoa mipya
nchini pamoja na makao ya nchi Dodoma.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, katika Bandari ya Mkoani katika
Mkoa wa Kusini Pemba, jana, Mhandisi Masauni alisema, ujenzi wa nyumba
hizo utakua ni wa hatua ya awali, lakini mipango mbalimbali itaendelea
kuwezesha nyumba nyingi zaidi kujengwa katika eneo hilo ili kuhakikisha
baadhi ya askari wanaoishi nje ya kambi za polisi waweze kuishi kambini
ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi
mkubwa zaidi.
“Leo
nimewakabidhi wakuu wa mikoa hawa vifaa vya ujenzi ambavyo ni mifuko ya
saruji, nondo, ndoo za rangi na mabati ili waweze kusimamia zoezi hili
la ujenzi wa nyumba za askari wetu kwa umakini mkubwa,” alisema Masauni
na kuongeza;
“Tunajenga
nyumba hapa Pemba ni mradi wa awamu ya kwanza, kwa awamu ya pili
tutaenda katika maeneo mengine ya nchi, hususani mikoa mipya yaSimiyu,
Geita, Katavi na Songwe na pamoja na Makao ya nchi Dodoma, kwa kuwa
askari wetu hawa wanafanya kazi kubwa sana kwa kuwalinda raia wa nchi
hii kuendelea kuwa salama kwa wao wenyewe pamoja na mali zao.”
Alisema
anawashukuru wadau mbalimbali kwa kujitolea kutoa vifaa hivyo ili
kufanikisha suala hilo na aliwataka watanzania wawe na moyo kama wadau
hao kwa kuipenda nchi yao, kupenda maendeleo kwa kutoa misaada
mbalimbali.
Masauni
alifafanua kuwa, suala la maendeleo halina siasa, tuijenga nchi, katika
mazingira mengi ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa maana ya Unguja katika
suala la kujitolea wamekua wanafanya hivyo, ila kuna changamoto kidogo
kwa upande waPemba pana tatizo la masuala ya kisiasa, watu wamekua
wakiingiza siasa mbele katika masuala ya nchi katika mikoa hiyo ya
Pemba, ambapo alisema jambo hilo sio jema katika maeneleo ya nchi.
“Serikali
zote mbili ya Bara na Visiwani zipo kuwahudumia wananchi wote, wakati
wa siasa umepita, sasa hivi tunataka kila mmoja ashiriki katika masuala
yote ya kimaendeleo, askari hawa wanaangalia usalama wa watu wote, bila
kujali hitikadi, dini ya mtu, wapi anatoka, bila kujali rangi yake bila
kujali kabila lake,” alisema Masauni.
Alisema
viongozi wa Serikali katika mikoa ya pemba wamekua wakipata tabu
kuhamasisha katika masuala mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao,
hivyo wao kama serikali kuu wameamua kupeleka maendeleo katika maeneo
ambayo yanakua yana tabu katika kuhamasisha masuala ya maendeleo, hivyo
wakaamua waje mikoa hiyo ya Pemba katika awamu hiyo ya kwanza ya mradi.
Akizungumzia
ujio huo wa Naibu Waziri pamoja na ujenzi wa nyumba hizo, Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla, alisema anamshukuru kiongozi
huyo kwa kuwaletea maendeleo hayo makubwa ya ujenzi wa nyumba za
polisina kumuhkikishia vifaa walivyopokea watasimamia ujenzi wa nyumba
hizo kwa nguvu zao zote.
“Sisi
wakuu wa mikoa tunakushuru naibu waziri kwa hili ulilolifanya,
tunakuhakikishia tutasimamia ujenzi huu kwa juhudi zote mpaka nyumba
zitakapokamilika, tunasema asante sana kwa kuhamasisha wadau na hatimaye
kufanikiwa kupata vifaa hivi,” alisema Mwajuma.
No comments:
Post a Comment