Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe Leo Novemba 11,
2017 ametembelea Vituo vya ukaguzi wa mazao vilivyopo Wilaya ya Rombo
Mkoani Kilimanjaro ili kujionea ufanisi wa utendaji kazi sambamba na
kubaini Changamoto zinazowakabili ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa
ushuru.
Katika
ziara hiyo ya kikazi Mhandisi Mtigumwe ametembelea Kituo cha HOLILI na
TARAKEA ambavyo vipo upande wa Tanzania ikiwa ni mpakani mwa Tanzania na
Kenya.HOLILI
ni moja ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya ambalo upo umbali wa
takribani Kilomita 25 Kutokea Himo Njiapanda huku Mpaka wa TARAKEA ukiwa
umbali wa Takribani Kilomita 58 kutokea Himo Njiapanda.
Miongoni
mwa Changamoto alizozibaini katika ziara hiyo kwenye Vituo vya ukaguzi
wa Kilimo kwenye hivyo mipaka miwili ni pamoja na uduni wa vifaa vya
kufanya kazi za Kiofisi, Kutokuwa na vifaa vya kufanya kazi ya kupimia
Sampuli ya mazao katika Maabara ya Holili.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mtigumwe amewataka watumishi
wanaosimamia ukaguzi wa mazao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji
Rushwa kwani kwa mtumishi atakayebainika kufanya hivyo sheria
zitachukuliwa haraka dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Mpaka huo wa TARAKEA una jumla ya Njia za panya 250 kutokea Mpaka wa Hororiri mpaka kufikia mpaka wa Namanga.Aidha,
Alisema serikali inaendelea na juhudi mbalimbali za kuzikabili Njia za
panya zote ili kubaini kila aina ya uhalifu unaofanywa ikiwemo magendo
yanayopitishwa kinyemela.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika
Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA kilichopo Katika Wilaya ya Rombo
Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika
Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo
Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisikiliza
maelezo ya utendaji kazi katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI
kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania
na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua maabara
ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI
kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania
na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akifungua bomba
ili kuona kama maji yanatoka wakati akikagua maabara ya upimaji wa mazao
katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya
Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Picha
ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI
kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania
na Kenya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John
Mtigumwe.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu
cha wageni Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya
kuwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA.
No comments:
Post a Comment