Askofu
“Atallah Hanna’ ambae ni Askofu Mkuu wa Sebastia wa Kanisa la Orthodox
la Kigiriki, amesema: "Uwepo wa Ukristo katika nchi hii takatifu
(Palestina), ni uwepo wenye historia ya tangu, kwani Ukristo haukuja
Palestina kutoka mahali popote duniani, bali umesambaa kutokea hapa
katika ardhi takatifu aliyoichagua Mungu,ili iwe ni sehemu ya upendo
wake kwa wanadamu".
Askofu
“Hanna”ameongeza kusema kuwa, "Tunatoa wito kwa watoto wetu wasome
historia ya kanisa lao na waelewe urithi wao wa kiimani, kibinadamu,
kiroho na kiuzalendo. Haifai kuwa hawaelewi historia na mizizi yao ya
kina (asili yao) iliyo katika udongo wa nchi hii takatifu. Tunaamini
kanisa moja ambalo ni chuo kikuu kitakatifu cha kiutume, lakini pia
tunajivunia kuwa sisi ni wana wa nchi takatifu ya Palestina. Tunajivunia
kuwa sisi ni wa nchi hii, historia yake, urithi wake na utambulisho
wake, huku tukitetea haki ya masuala ya wananchi wake."
Aidha
amesema "Katika kumbukumbu ya azimio baya la Balfour, upendeleo wetu
utabaki daima na wananchi wa Palestina na kwamba kuvamiwa Palestina
kumetokana na azimio la Balfour na wala hakukutokana na Mungu. Hatuwezi
kuwakubalia wale wanaomnasibisha Mungu na jambo ambalo sio lake, wala
kuwakubalia wale wanaofasiri Biblia kama wapendavyo, hatimae wakasema na
kuhalalisha alichokiharamisha Mungu.”
“Tunaamini
kwamba Mungu hakuhalalisha mauaji, vurugu, kuhamisha watu kwa nguvu na
matendo ya kukiuka Utu na hadhi ya kibinadamu, tunaamini kwamba maadili
haya yapo katika dini tatu za kumpwekesha Mungu. Katika imani yetu ya
kikristo na kwa mujibu wa maadili yetu ya kiinjili, tunasema haifai
kudhulumiwa au kukandamizwa binadamu yeyote, yale yaliyotokea mwaka 1948
ya kuwatoa kwa mabavu Wapalestina katika makazi yao, miji yao na ardhi
yao takatifu, sio haki kwa njia yoyote.”
“Yanayofanywa
na baadhi ya makundi ya kiimani ya kizayuni nchini Marekani na sehemu
nyingine ambayo yanalihusisha tukio la mwaka 48 na dini, tunawaambia
kwamba kilicholitokea taifa letu hakipo hivyo kwa njia yoyote, tunapinga
mtu kututafsiria Biblia kwa njia isiyofaa na kwa kuzingatia athari za
kizayuni. Hawa wanaharibu maadili na ujumbe wa Kikristo katika ulimwengu
wetu huu, ambavyo vimekuwa na daima vitaendelea kuwa ni ujumbe wa
upendo, undugu, amani na upendeleo wa wenye kudhulumiwa na wenye kuteswa
katika dunia hii.”
Askofu
“Atallah Hanna’ ameongeza kusema kwamba "Sisi kama Wakristo na Waislamu
kwa pamoja tunaitetea Jerusalemu, sehemu zake takatifu na wakfu
zake,huku tukiomba zifeli njama zote dhidi yetu bila kumbagua yeyote
kati yetu.
Askofu
ameyasema hayo asubuhi ya siku ya Novemba 2, alipokuwa akipokea ujumbe
wa kikristo kutoka eneo la “Acre” upande wa kaskazini, uliotembelea
Kanisa la Ufufuo na kukutana nae. Ujumbe huo umeelezea heshima na
shukrani zao kwa uwepo wa Askofu na utetezi wake kwa Jerusalemu, sehemu
zake takatifu na wakfu zake, vilevile utetezi wa kudumu wa Askofu katika
uwepo wa kikristo kwenye kitongoji hiki takatifu duniani.”
Aidha,
katika mapokezi hayo pia yalijadiliwa mambo kadhaa likiwemo suala la
Jerusalemu na vilivyomo pia uwepo wa kikristo katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment