A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, October 2, 2017

Wazee wa CHADEMA wamtolea kaulii hii Rais Magufuli


Baraza la Wazee wa CHEDEMA likiongozwa na Katibu mkuu wao , Roderick Lutembeka wamefunguka na kumshauri Rais Magufuli kuwa anapaswa kukutana na wazee mbalimbali pamoja na viongozi wastaafu ili waweze kumshauri na yeye kufanyia kazi ushauri wao. 

Roderick Lutembeka alisema hayo jana katika siku ya Wazee Kimataifa ambayo huadhimishwa kila Oktoba Mosi ya kila mwaka na kusema kuwa Rais anapaswa kukutana na wazee hao ili waweze kumshauri na kusema kuwa watu ambao wamemzunguka Rais sasa hawawezi kumwambia ukweli kwa kuhofia kupoteza nafasi zao. 

"Tunatoa wito kwa Rais Magufuli kukutana na Wazee katika kikao cha pamoja ambao hawataogopa kumwambia ukweli ili tuliepushe taifa na madhara makubwa yanayoweza kulipata. Wazee ambao tunashauri Rais Magufuli akutane nao katika kikao cha pamoja ni pamoja na wazee kutoka vyama vya siasa, viongozi wastaafu wa dini mbalimbali nchini, wastaafu serikalini, na awe tayari kusikiliza na apokee ushauri na ukosoaji wao kama ambavyo anasikiliza na kupokea hongera" alisema Lutembeka 

Aidha kiongozi huyo aliendelea kwa kusema "Kwa sababu tunajua waliomzunguka kwa sasa hawawezi kuthubutu kumwambia ukweli kupitia ushauri wao kwa sababu wanalinda vyeo vyao na pengine wanajua yaliyowapata wenzao waliyojaribu kusema ukweli" 

Mbali na hilo Wazee hao wa CHADEMA walitoa ushauri kwa wazee wengine nchini na kuwataka kuendelea kutoa ushauri wao na kukosoa pale inapostahili bila kuogopa pamoja na kukemea mwenendo wa nchi. 

"Tunapenda kutoa wito kwa Wazee wote bila kujali tofauti zozote zile wasimame imara na kujitokeza hadharani kukemea mwenendo mbaya wa nchi yetu ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu, ukiukwaji wa sheria na Katiba ya Nchi, kauli na matendo mabaya yanayozua sintofahamu kubwa kwa Watanzania.Kutoa ushauri bila kuchoka kwa watu wote hasa kwa vijana wetu na viongozi wenye mamlaka. Kushiriki kikamilifu katika kuendelea kuwatengenezea nchi Wazee wa kesho (vijana au watu wazima wa leo), hasa kudai Katiba Mpya" alisema Roderick Lutembeka

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages