Washindi
wa michuano ya Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika Octoba 29
mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wanatarajiwa
kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 40 pamoja na
medali, imefahamika.
Akizungumzia
zawadi hizo jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo kutoka
kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe alisema
pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume
na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa
washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi
wanne hadi kumi na tano nao pia wakiibuka na zawadi za medali na pesa
taslimu.
Kwa
upande wa mbio za Kilomita 21, Bidan alisema pamoja na medali washindi
wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 2/- kila
mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. Laki 5/- kwa washindi wa
tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi
za pesa taslimu na medali kila mmoja.
“Mbio
za kilomita tano tunatarajia kwamba zitaongozwa na Waziri wa Maliasili
na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, baadhi ya wakuu wa mikoa kutoka kanda
ya Ziwa huku pia zikihusisha wadhamini wa mbio hizi kutoka mashirika
mbalimabli yaani(Corporates).’’ Alisema.
Aidha
wadhamini ambao pia watashiriki katika mbio hizo ni pamoja na kampuni
za Tiper, Puma Energy, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro, New Mwanza Hotel, Real PR Solutions, Efm Radio, EF Out
Door, CF Hospital na Afrimax Strategic Partnerships Limited.
Alibainisha
kuwa mbio hizo za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani
Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za
utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa
washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
Alisema
washindi wa mbio za Kilomita tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya
wazee watapatiwa sh 100,000/- kwa washindi wa kwanza huku washindi wa
pili wakipata sh 70,000/ na watatu wakipatiwa sh 50,000/-pesa taslimu.
“Kwa
washindi wa mbio za kilomita mbili na nusu zitakazohusisha watoto wenye
umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa sh 50,000/-kila mmoja huku wa
pili na watatu pia wakipatiwa pesa taslimu.’’ Aliongeza
Zaidi
aliongeza kwamba washindi kwanza kwenye mbio fupi za uwanjani za mita
100,200, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi watapatiwa
zawadi ya sh 50,000/ kila mmoja (wanaume na wanawake), sh 30,000 kwa
washindi wa pili huku washindi watatu wakiambulia kiasi cha sh 20,000
kwa kila mmoja.
Akizungumzia
usajili wa mbio hizo Bw. Bidan alisema kwa wakazi wa jiji la Mwanza na
mikoa jirani wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika vituo kadhaa
vikiwemo Ofisi za michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi zote za
riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga, Uwanja wa Nyamagana, Chuo
Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Kituo cha michezo Malya, Shule
ya Kimataifa ya Isamilo, New Mwanza Hotel na Ofisi za EF Out door
zilizopo jingo la Rock City Mall.
“Kwa
upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi
za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya sita jengo
la SHAMO Tower, Mbezi Beach , jijini Dar es, Salaam na EFM Jogging Club
iliyopo Coco Beach Dar es Salaam” alitaja.
Zaidi
kuhusu usajili wa mbio hizo zinazoandaliwa kwa kushirikiana na Chama
cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Bidan alisema unaweza kufanyika
kupitia tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni www.capitalplus.co.tz
Alitoa
wito kwa washiriki zaidi kujisajili ili kuthibitisha ushiriki wao
kwenye mbio hizo ambazo mbali na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha hapa
nchini pia zinalenga kupambana na ujangili pamoja na kutangaza utalii
katika mikoa iliyopo Ziwa ya Ziwa.
No comments:
Post a Comment