Watanzania
wametakiwa kuenzi mila na desturi ambazo ni chanya wazitunze na
kuzitumia ili kujenga jamii yenye maadili mema nchini kwa manufaa ya
kizazi cha sasa na baadaye.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Anastazia Wambura alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni
(4CCP) Haydom wilaya Mbulu mkoani Manyara ambapo amejionea utajiri wa
kiutamaduni wenye fursa za utalii wa kiutamaduni.
“Nimetembelea
nyumba za asili zilizopo hapa katika kituo hiki nimefurahishwa sana na
utajiri wa kiutamaduni uliopo hapa, wazee walizingatia maadili katika
kuwalea watoto wao kulingana na mila na desturi zao, ni vema tuenzi
utamaduni wetu, huo ni msingi wa maadili mema ya jamii” alisema Naibu
Waziri Wambura
Akitolea
mfano wa maadili mema yanayopaswa kurithishwa aliyojionea katika kituo
cha 4CCP na namna ambavyo watoto waliheshimu nyumba za wazazi wao, Naibu
Waziri Wambura amesema kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzani
suala la ulevi na utumiaji wa tumbaku kwa vijana ilikuwa ni mwiko hadi
kijana afikie umri wa utu uzima ambapo anaweza kuwa na maamuzi sahihi
katika maisha yake yenye kuwa na tija kwa familia.
“Kabla
ya kuoa kijana alikuwa haruhusiwi kutumia tumbaku na kunywa pombe, bali
kijana akioa na kuwa na watoto wawili kwa mujibu wa mila za makabila ya
yaliyopo Mbulu aliruhusiwa kuingia katika kundi la watu wazima na
kuruhusiwa kutumia vitu mbalimbali ikiwemo tumbaku na kinywaji cha
pombe. Hapa kuna jambo la Watanzania kujifunza na kutunza ili kuondokana
na mmomonyoko wa maadili” alisema Naibu Waziri Wambura.
Mila
za jamii zilizo njema zinapaswa kutunzwa na kuendelezwa ili ziweze
kusaidia vijana na jamii kwa ujumla kuweka mawazo yao katika shughuli za
maendeleo pamoja na kupatia familia zao mahitaji ya kila siku.
Naibu
Waziri Wambura alisisitiza kuwa mila hizo hazitakiwi kuachwa bali
zainatakiwa kuenziwa, kutunzwa, kuendelezwa na kuhifadhiwa kwa manufaa
ya sasa ziweze kuchangia katika kukuza utalii wa kiutamaduni ambao ni
moja ya vyanzo vya mapato kwa wanajamii na taifa kwa ujumla.
Aidha,
Naibu Waziri Wambura alisema kuwa wilaya ya Mbulu ni tajiri katika
masuala ya utamaduni na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni mdau muhimu katika
sekta ya michezo na utamaduni ambazo zinapaswa kuendelezwa kwa manufaa
ya taifa.
Kwa
upande wake Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay amesema kuwa wilaya
hiyo imekuwa na utamaduni wa kufanya tamasha la utamaduni kila mwaka
ambapo mwaka huu lilifanyika tarehe 21 hadi 23 mwezi Septemba na
inaedelea kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa jamii
katika masuala mbalimbali ya maendeleo hatua inayopelekea makabila yote
kuwa mstari wa mbele katika kudumisha amani ya nchi.
Mbunge
huyo aliyataja makabila yanayotokana na makundi makuu manne
yanayopatikana wilaya ya Mbulu kuwa ni pamoja na Wairaqw ambao ni jamii
ya Wakushi, Wahadzabe jamii ya Khoisan, Wanyiramba na Wanyisanzu jamii
ya wabantu na Wadatooga jamii ya Kiniloti.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga amemhakikishia Naibu Waziri
Wambura kuwa wilaya hiyo itaendelea kuenzi sekta ya utamaduni kwa kuwa
na tamasha la utamaduni linalokutanisha makabila yote wilyani humo
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani ambayo
hufanyika mwezi Mei tarehe 21 kila mwaka.
Hatua
hiyo inatokana na Tanzania kusaini mkataba wa azimio la Umoja wa
Mataifa (UN) kuenzi utamaduni na kuheshimu tamaduni za watu wengine
chini unaosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO).
Mwaka
2002 Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha maadhimisho ya siku ya
Utamaduni Duniani kutokana na kuongezeka kwa migogoro, mapigano na
kupotea kwa maisha ya watu na mali zao iliyokuwa inatokea sehemu
mbalimbali duniani mwishoni mwa miaka ya 1990.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi
na Usalama mara baada ya kuwasili Wilayani Mbulu kwa ziara ya kikazi ya
siku mbili wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akimkaribisha Naibu Waziri wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura kuongea
na wananchi waliokuwa katika tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe
Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa
ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.
Baadhi
ya Washiriki wa tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za
Utamaduni (4CCP) Haydom, wilaya ya Mbullu wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (hayupo
pichani) alipotembelea kituo hicho.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura akitoka ndani kujionea moja ya nyumba za asili ya Wabantu
Wanyiramba na Wanyisanzu iliyopo Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP)
kilichopo Haydom.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura akicheza ngoma na washiriki wa tamasha la utamaduni
alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura (wa pili kulia) akipata maelezo ya utamaduni wa kabila la
Wadatoga katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo
Haydom.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia
Wambura (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasichana wa
kabila la Datoga na kusisitiza Watanzania kuenzi utamaduni wetu kwa
kuurithisha kwa vijana wetu. Wa nne kushoto ni Mbunge wa Mbulu Vijijini
Flatei Massay
No comments:
Post a Comment