A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 1, 2017

RC MAKONDA KUJENGA OFISI ZA KISASA 402 ZA WALIMU

 Picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo ya ujenzi na uboreshwaji wa ofisi za waalimu kwa mkoa wa Dar es salaam akiwa pamoja na Afisa elimu wa mkoa aliyevaa koti.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  leo ametambulisha Kamati ya Ujenzi wa  Ofisi za Kisasa 402   za Walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari zilizobainika kukosa Ofisi hizo.

Kamati ya ujenzi wa Ofisi za Walimu itaongozwa na Mwenyekiti  Canal Charles  Mbuge  kutoka JKT,Makamu Mwenyekiti  ACP.Solomon Urio  kutoka Jeshi la Magereza, Katibu wa Kamati ambae pia ni Afisa Elimu wa Mkoa   Hamis  Lissu ,Katibu Msaidizi  SACP Juma  Hamis   kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Wajumbe.

Makonda  amesema Ujenzi wa Ofisi hizo utaanza  September 05  chini ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka  JKT, Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza  walioamua kuunga Mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa.

Amesema kuwa hadi sasa JKT wametoa Vijana 300  kwajili ya ujenzi huo huku Jeshi la Magereza likitoa Wafungwa watakaofanya kazi ya kutengeneza  Matofali.

Aidha Makonda  amewaomba  Wadau na Wananchi  kuchangia Fedha na vifaa ikiwemo  Mabati, Nondo, Saruji, Kokoto, Mchanga, Mbao na Nguvu kazi ya Watu  ilikuwafanya Walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri.

Amesema kuwa Wananchi wanaweza kuchangia fedha kupitia Account ya
CRDB namba 0150296180200  au kuwasilisha michango yao Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Katika ujenzi huo  Channel Ten  wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuhamasisha Jamii katika uchangiaji.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages