A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, September 26, 2017

WANAWAKE WAJASIRIAMALI JITOKEZENI KWA WINGI KUSHIRIKI TAMASHA LA MWANAMKE MJASIRIAMALI

Mwenyekiti wa Tamasha la mwanamke mjasiriamali (MOWE),Zubeida Kiluwa wa pili(kushoto),akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la mwanamke mjasiriamali  litakalofanyika mnazi mmoja ocktoba mwaka huu hafla hiyo imefanyika leo jijini dar es salaam.
 Mjumbe wa kamati ya (MOWE) Anna Matinee (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.
Blandina Sembu (kulia), akizungumza kuhusiana na tamasha hilo. picha na Brian Peter
 

Wanawake wajasiriamali nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho ya tamasha la mwanawake wajasiriamali "Month of Women Entrepreneus"(MEWO) litakalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam kwanzia tarehe 24 hadi 30 October mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mwenyekiti wa tamasha la mwanamke mjasiriamali (MOWE) Zubeida Kiluwa amesema wanawake wajasiriamali wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha wanawake wajasiriamali na kuweza kupata fursa ya masoko na kuweza kuuza bidhaa zao,na kupitia tamasha hili lenye kauli mbiu isemayo "Mwanamke Mjasiriamali Funguka Shiriki Kumjenga Tanzania ya Viwanda".

Aidha amesema mgeni rasmi katika tamasha hill ni Waziri wa viwanda  na biashara Mh. Charles Mwijage, na pia amewakaribisha wananchi wrote kushiriki kwenye maadhimisho hayo kwa kuweza kujipatia bidhaa mbalimbali kutoka kwa wanawake wajasiriamali wa hapa nchini na kutoka nchi jirani.

Kwa upande wake mjumbe wa tamasha la mwanamke mjasiriamali(MOWE) Anna Matinde amewataka wanawake wote wajasiriamali na vikundi mbalimbali vya mjasiriamali kushiriki vyema katika  tamasha hilo ambapo gharama ya kushiriki katika maonesho hayo ni shilingi 50,000 kwa siku zote za maadhimisho ya tamasha.

" Wananchi wote watakaoingia katika maadhimisho hayo katika viwanja vya mnazi mmoja kwa ajili ya uzinduzi,ununuzi na kujionea bidhaa mbalimbali hakutakuwa na kiingilio chochote wanakaribishwa bure tamasha" amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages