Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Bi. Mtanga Noor (kulia), akiwapokea baadhi ya wahariri wa habari wakati wa ziara ya wahariri wa habari za biashara na uchumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Pongwe, Tanga juzi kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji saruji , mipango ya maendeleo na changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Reinhardt Swart (kulia, akizungumza wakati wa ziara ya wahariri hao walipotembelea kiwandani hapo, Pongwe, Tanga juzi kujionea shughuli za uzalishaji wa saruji na mipango ya maendeleo ya kampuni hiyo.
Mmoja ya waandishi wa habari mkoani Tanga, Mngazija akijitambulisha wakati wa ziara hiyo.
Baadhi ya maofisa na wataalamu wa Kampuni ya Saruji Tanga wakiwa tayari kutoa elimu kuhusu uzalishaji saruji na kujibu maswali wakati wa ziara hiyo.
Meneja Usambazaji wa TCPLC, Samuel Shoo (kulia), akitoa elimu kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji saruji na ubora wake kwa wahariri hao.
Baadhi ya wahariri wa habari za biashara na uchumi wakiwa katika chumba cha kuendeshea mitambo cha kampuni hiyo.
Meneja Machimbo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Godwin Kamando (kulia), akitoa maelezo kuhusu shughuli za uchimbaji mawe katika eneo la machimbo ya kampuni hiyo wakati wahariri wa habari za biashara na uchumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Pongwe, Tanga juzi kujionea shughuli za uzalishaji wa saruji.
No comments:
Post a Comment