A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, August 10, 2017

RC MAKONDA AAGIZA CV ZA WATENDAJI KATA DSM KUPITIWA UPYA

RC Makonda aagiza CV za watendaji kata za jiji la Dar es Salaam kupitiwa upya hatua hiyo imefuata baada ya Mkuu huyo wa Mkoa D ar es Salaam  kufika katika eneo la Bunju B jijini humo kwa maelekezo ya Rais Magufuli aliyetoa siku 4 kutatuliwa kero za eneo hilo.

Katika mkutano na wananchi wa eneo hilo, RC Makonda alilazimika kumuinua mtendaji wa kata hiyo na ndipo alipogundua wengi wao hawaelewi vizuri majukumu yao na ndipo alipomuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Ally Happi kukagua CV za watendaji wake mara moja.

RC Makonda amedai Watendaji hao kutoelewa majukumu yao ndio imekuwa sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero ndogondogo na hatimaye Wanasubiri Rais akipita wanamsimamisha kwa matatizo madogodogo yakiwemo ya Vyoo, Umeme na masoko.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi (kushoto) akizungumza na waanchi wa Bunju B akifafanua jambo katika mkutano huo.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages