Mkurugenzi wa Shule zote za Al Muntazir Mohamood Ladak akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mdahalo unaofanyika katika Shule yake iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakishiriki kikamilifu katika mdahalo unaendelea kufanyika jijini Dar es Salaam katika shule ya seminary ya AL Muntazir.
Baadhi wa wanafunzi wakikiliza kwa umakini mada iliyokuwa ikichangiwa na wanafunzi katika mdahalo (Bedate).
Mmoja wa washiriki katika mdahalo huo akiongea jambo mbele ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Zaidi Wanafunzi 250 wa Sekondari kutoka nchi mblimbali barani Afrika weanaza Mashindano ya mdahalo (Debete) yanayofanyika katika shule ya Al Muntazir Seminary iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi jinsi ya kijieleza, kujiamini jambo ambalo linaweza kuwasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Shule zote za Al -Muntazir Islamic Mahmood Ladak, amesema kuwa katika mashindano hayo kuna jumla ya shule 15 kutoka Tanzania, huku nyingine zikitoka nchini Zimbambwe, Afrika ya Kusini pamoja na Uganda.
Ladak amesema kuwa kwa lengo la mashindano hayo ni kuwakutanisha wanafunzi wa kitanzania na wezao kutoka kutoka nchi mbalimbali ili kubadilishana mawazo ya kielimu waliojifunza darasani.
Amesema kuwa mashindano hayo yanajulikana kwa jina ‘Mwalimu Nyerere School Inventation Debete Championship’ yanayotarajiwa kumalizika Agosti 13 mwaka huu.
Amefafanua kuwa miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika mdahalo huo ni pamoja na mfumo wa kimataifa (National system) pamoja na matukio mbalimbali.
“Kuna mada mbalimbali ambazo wanajadili ikiwemo na mada zinazohusu masomo kwani zinawapa fursa wanafunzi kubadilishana ufahamu wa kimasomo” amesema Ladak.
Naye Mratibu wa Taasisi inayojiusisha na masuala ya mdahalo (Debete) Dominic Mwakifulele, amesema kuwa katika kufanikisha mdahalo huu walitumia utaratibu wa wa kuwaandikisha shule ambazo zitashiriki (Process registration) kupitia kampeni ya mitando ya kijamii, pamoja na vyombo vya habari.
Hata hivyo baadhi ya wanafuzi kutoka shule mbalimbali wameonekana kufurai mdahalo huo ambao unawajenga kiakili.
Mduduzi Mhlanga ni mwanafunzi kutoka Shule ya St John Collage nchini Zimbabwe amesema kuwa mashindano hayo ni mazuri kwani yanawajenga katika kujieleza na kujiamini katika masomo yao.
Naye mwanafuzi Hawa kutoka Shule ya Al Muntazir Islamic Seminary ameushukuru uongozi wa shule anayosoma kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yameonekana ni rafiki kwa wanafunzi.
Bill Bob Luomba ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Al-Muntazir amesema kuwa ni fursa kwao katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika mdahalohuo.
Amesema kuwa mada mbalimbali zinaendelea kujadiliwa katika shule anayosoma ambayo imeonekana kiwapatia wanafunzi wake fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo ili waendelee kufanya vizuri.
Miongoni mwa shule zinazoshiriki kutoka Tanzania ni pamoja na Al Muntazir Islamic Seminary ambao ni miongoni mwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo yanafanyika nchini Tanzania mara ya pili.
Washiriki wa mashindano hayo ni shule za watu binafsi (Private) kutokana na kile kinachodaiwa wanafunzi wengi wa shule za Serikali wamekuwa wakikabiliwa na hofu ya kutoongea kiingireza.
No comments:
Post a Comment