Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda (wa pili kushoto) akizungumza na wananchi wa Tuangoma
wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam na kusitisha bomoa bomoa iliyokuwa
ikiendelea katika eneo hilo. Pia amewaomba kujiepusha na kujenga nyumba
za kuishi katika maeneo hatarishi. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya
Tuangoma wilaya Temeke, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe
Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda WAMESITISHA
zoezi la BOMOA BOMOA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba (17, 000)
zilizotangazwa KUBOMOLEWA na Baraza la Hifadhi ya Mazingira NEMC.
Hatua ya kusitisha zoezi hilo, Imekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Mhe Paul Makonda KUZUNGUMZA na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
kuhusiana na Sintofahamu ya bomoa bomoa hiyo ambayo AMEMUELEZA Mhe Rais
Magufuli kuwa Taarifa za BOMOA BOMOA ya Nyumba elfu kumi na saba iliyotolewa
HAIKUFIKA ofisini Kwake Jambo ambalo ni tofauti na Taratibu za Utendaji kazi wa
Serikali.
Mhe Makonda amesema, hata kama TAMKO hilo limetolewa na
watumishi wa Mkoa mfano Wakurugenzi wa Manisapaa au Wakuu wa Wilaya walioko
Chini ya Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa LAZIMA Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
IPATE TAARIFA na IRIDHIE bomoa bomoa hiyo, na pia hata kama Taarifa zimetoka
WIZARANI inapaswa taratibu za KIMAANDISHI zifuatwe kwa kujulisha Ofisi ya Mkoa.
"haiwezekani mtu kutoa TAMKO la kuvunja Nyumba elfu kumi na
saba bila Mkoa kujua, hilo HALIWEZEKANI" amesema Mhe Makonda.
Mhe Makonda amefafanua kuwa AMEONGEA na Mhe Rais Magufuli na
Kumuuliza kama ana taarifa za zoezi la Ubomoaji wa Nyumba elfu kumi na saba
ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ALIMUELEZA Mhe Rais
Magufuli kuwa HANA taarifa hizo za UBOMOAJI, zaidi Ubomoaji wa Nyumba zilizo
kwenye Hifadhi ya Barabara ya kuanzia Ubungo kwenda KIMARA na MBEZI Ubomoaji
unaofanywa kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Morogoro, Ubomoaji wa Nyumba
zilizo Jirani na Reli hususani ni zile zinazohusiana na Ujenzi wa Reli Mpya na
ya Kisasa.
Kutokana na Sababu hizo, Mhe Makonda amesema Mhe Rais
amesikitishwa na TAMKO hilo la kutaka KUBOMOLEWA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi
na saba na ametoa pole kwa Wananchi waliokumbwa na TAHARUKI ya TAMKO hilo la
Ubomoaji, na kusisitiza kuwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAKUCHAGULIWA
kwa ajili ya KUBOMOA Nyumba za watu na kusisitiza kuwa anataka wananchi
WANAOISHI katika maeneo HALALI kuachwa mana AMEPATA taarifa kuwa huenda ZOEZI
hilo lingekwenda mbali zaidi mpaka kwa Wananchi WASIOHUSIKA.
Katika HATUA nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul
Makonda AMEPIGA MARUFUKU zoezi lolote UBOMOAJI wa Nyumba pasipo Ofisi yake
kupewa TAARIFA na kisha KURIDHIA Ubomoaji huo.
Mwisho, Mhe Paul Makonda AMEWATAKA wananchi na wakazi wote wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuzingatia SHERIA na wasivamie maeneo au kuuziwa VIWANJA
na Matapeli na pia AMEWATAKA wananchi kuchukua TAHADHARI hususani ni katika
maeneo yote HATARISHI ambayo sio SALAMA kwa MAKAZI na kuwataka kila Mwananchi
Mwenye Familia KUTAFUTA Salama kwa Maisha yake na ya Familia yake.
Mhe Makonda Pia ametoa OMBI Maalumu Kwa Waziri Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi la KUBORESHA mfumo wa Ardhi katika Mkoa
wa Dar es Salaam kwa kuanzisha mpango wa kuweka MAAFISA ARDHI katika KATA zote
za Mkoa wa Dar es Salaam ambao watakuwa na JUKUMU la KUSIMAMIA, KURATIBU
masuala yote ya Ardhi ngazi ya KATA hatua ambayo itasaidia kuondoa Migogoro na
UTAPELI kwa Wananchi kuuziwa au kununua Ardhi katika maeneo ambayo
HAYARUHUSIWI, ambapo amesema amepata wazo hilo kutokana na uzoefu aliopata
akiwa Rais wa umoja wa Vyuo vikuu -TAHILISO ambapo alishirikiana na Bodi ya
Mikopo kuanzisha mfumo wa kuwa na MAAFISAMikopo katika vyuo hatua
iliyosababisha kuondoa kero ya wanafunzi kufuatilia Mikopo katika Ofisi za bodi
ya Mikopo hatua ambayo imekuwa mwarobaini wa tatizo la kufuatilia Mikopo kwa
wanafunzi, Mhe Makonda amesema atamwandikia OMBI hilo na kulifikisha Rasmi kwa
Mhe Lukuvi ili amsaidie kulifikisha kwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa
ajili utekekezaji.
No comments:
Post a Comment