Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Paul Makonda* leo ametangaza kuanza kwa *Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwaajili ya Wananchi 1,000* wenye uhitaji wa Miguu hiyo ilikuwawezesha kutembea na kufanya shughuli zao.
Katika zoezi hilo Wananchi wataweza kutoa Michango yao kwa njia ya *Simu, Bank au kufika Ofisi za Mkuu wa Mkoa* na kuwasilisha michango yao.
Hatua hii inakuja baada ya wenye uhitaji wa *Miguu Bandia*kuwa kubwa tofauti na ile iliyokusudiwa na Mkuu wa Mkoa ya watu 200 ambapo awamu ya kwanza jumla ya watu *650* walichukuliwa vipimo.
*Makonda* amesema bado uhitaji wa Miguu hiyo ni mkubwa hivyo amewaomba wadau ikiwemo *Makampuni, Taasisi na Watu Binafsi* kujitokeze kuchangia ili kutimiza dhamira yake ya kuwafanya walemavu kutembea.
Hadi sasa Wadau mbalimbali ikiwemo *CCBRT* wamechangia *Miguu 25* kwaajili ya Miguu ya watu wenye Ugomjwa wa Kisukari,Msanii *Mrisho Mpoto* miguu mitatu huku Taasisi za MOI, Ajma Othopedics Medical Service wakiunga mkono zoezi hilo.
Baada ya kuona uhitaji ni mkubwa wa Wananchi Kituo cha Utangazaji cha *EFM na TV E* wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbal
No comments:
Post a Comment