Wananchi
365 wa kijiji cha Chongoleani watafidiwa shilingi bilioni 3,035 kwa
ajili ya kutoa maeneo yao, ili kupisha ujenzi wa bomba la mafuta
linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga.
Hayo
yamesemwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Usimamizi wa Bandari
Tanzania TPATanga, Bibi Janeth Rwuzangi katika mahojiano maalum leo.
Bi Ruzangi amesema kuwa kwa hapa Chongoleani mradi
una ukubwa wa hekta 200 zikiwemo hekta 100 zitakazotumiwa kuweka
miundombinu ya mafuta ghafi. Hekta 100 zilizosalia zitatumika kwa ajili
ya shughuli za TPA) kuwekeza miundombinu ya kupokea mafuta
yaliyosafishwa. Vile vile eneo hili limezingatia maendeleo endelevu ya
biashara ya mafuta na gesi katika siku zijazo
Aliongeza
kuwa TPA itakuwa na wajibu wa kuhudumia meli, kuhakikisha usalama wa
bidhaa, vyombo na watu pamoja na kusimamia masuala ya afya bandarini.
Aidha, Majukumu la TPA yanatarijiwakujikita katika shughuli za
uendeshaji wa majini ikiwemo kuwa na vyombo na boti maalumu kwa ajili ya
kuongozea meli wakati wa kuingia na kutoka kwenye gati la mafuta
ghafi.
Akitoa
ufafanuzi, Bi Ruzangi amesema vile vile, TPA ina jukumu la kuhakikisha
inahudumia shehena ya vifaa vyote vya ujenzi katika Bandari ya Tanga kwa
kushirikiana na Bandari Kuu ya Dar es Salaam. Shughuli nyingine ni
pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majini pamoja na usalama wa eneo la
Bandari ambalo limegawanyika katika sehemu kuu mbili; ardhini kwenye
gati la mafuta na majini kwenye lango la kuingilia meli na nangani.
Kwa
upande wa ajira za TPA Ruzangi amesemawafanyakazi ambao wataajiriwa ni
pamoja na mabaharia, wahandisi, mafundi, wahasibu, wachumi, watakwimu,
vibarua mbalimbali kwa ajili ya nguvu kazi n.k. Sehemu ya wafanyakazi
hawa watatokana na waliopo sasa kwenye Bandari watakaopangiwa kazi hizo.
Hata hivyo TPA inatarajia kuajiri wengine ambao watalazimika kufanya
kazi hizo kulingana na taratibu za ajira za TPA.
Pamoja
na kuwa na bomba la mafuta, kijiji cha Chongoleani kitafaidika na
ujenzi wa barabara ya kilometa 8 itakayounganisha bandari na barabara
kuu ya Horohoro – Tanga, ambapo kwa kiasi kikubwa itainua uchumi wa
wananchi wanaoishi maeneo hayo kusafirisha mazao, samaki na bidhaa
nyingine kwa urahisi.
Akifafanua
uwekaji wa jiwe la msingi Ruzangi amesemakuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli na Mgeni wake Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni wanatarajia kuweka jiwe la msingi la Mradi
wa Bomba la Mafuta tarehe 05 Agosti 2017.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Chongoleani, Bw. Mbwana Nondo amesema; “Kwa
moyo wa dhati kabisa, naomba nimshukuru sana sana Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kutujali wananchi wake
na kutuletea neema ya Mradi wa Bomba la Mafuta, katika maisha yetu
wanachongoleani, hatutaweza kumsahau kwa kizazi hiki kinachoshuhudia
mradi huu na vizazi vijavyo”.
Nondo
alisema kuwa anamuhakikishia Mhe. Rais kuwa kuwa wote watakaopata
fursa kwenye mradi wa Bomba la Mafuta, watafanyakazi kwa bidii ili
kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Bomba
la Mafuta la kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Chongoleani lina urefu wa
Kilometa 1445 ambapo kwa upande wa Tanzania itakuwa na jumla ya kilometa
1115 na Uganda 330. Aidha, Mradi utatarajia kusafirisha mapipa laki
mbili na kumi na sita elfu (216,000) kwa siku .
Kijiji
cha Chongoleani ndio kituo cha mwisho ambapo mitambo mikubwa itasimikwa
katika eneo hili kwa ajili ya kusukuma mafuta eneo la baharini
ili, kuweka kwenye vyombo vya usafirishaji kusafirisha maeneo
mbalimbali duniani ambayo Uganda watakuwa wamepata soko.
Tanzania
itafaidika na mradi huu kutokana na kodi, tozo na mrahaba wa bomba la
mafuta, itakayofanywa moja kwa moja na mradi huo. Faida nyingine ambazo,
sio za moja kwa moja ni ajira, fursa za kufanya biashara na uwezekano
wa mikoa 8 ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma,
Morogoro na Tanga.
No comments:
Post a Comment