A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, August 13, 2025

AGRA, Sahara Accelerator kunufaisha vijana wengi kupitia kilimo

Na Mwandishi Wetu

Kilimotech Accelerator kupitia Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture (YEFFA) inayodhaminiwa na shirika la AGRA Tanzania na kutelekelezwa na Sahara Accelerator inatarajia kunufaisha vijana wapatao 265,000 wanaojihusisha na masuala ya kilimo.

Akizungumza wakati wakijadili na vijana kuhusu fursa hiyo jijini Dar es Salaam, Adam Mbyallu wa Sahara Accelerator alisema fursa hiyo itatoa kiasi cha dola milioni 20 kwa bunifu za kilimo zinazojumisha mnyororo wa thamani kwa mazao manne ambayo ni mbogamboga na matunda, alizeti, mpunga na mahindi.

"Tuna hakikisha namna gani tunaweza kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kilimo kupitia teknolojia za kidigitali tunasaidia vijana wenye bunifu mbalimbali zinzojibu changamoto za upatikanaji wa vifaa za kilimo," alieleza Mbyallu.

Alisema kupitia bunifu hizo watawapatia vijana hao mafunzo,mentorship na kuwaunganisha wa wadau mbalimbali na kusaidia kwenda shambani kwenye kilimo na kujiuza.
Alifafanua kuwa bunifu wanazotafuta zitajibu changamoto za kilimo kama vifaa,mafundi,masoko,udhibiti wa mazao,uharibifu wa mazao baada ya mavuno changamoto ambazo wadau wa kilimo walisema zipo.

"Maeneo hayo yote kama vinavifaa vya kilimo vingesaidia sana vijana kujiajiri kwenye kilimo kama watajiajiri tunaangalia jinsi ya kuwawezesha kupitia teknolojia ya kidijitali," aliongeza.

Mbyallu alisema ili kufanikisha upatikanaji wa bunifu hizo wamefungua dirisha la usajili wa bunifu kwa muda wa miezi miwili ambapo itafungwa Agosti 18, 2025 na zitachujwa kuangalia kama bunifu hizo zinakidhi vigezo na baada ya hapo watawaunga mkono.

"Tutawaunga mkono Kwa mafunzo,mentorship,changamoto na kuwaunganisha na wadau watakaowasaidia bunifu zao kwenda soko kama wadau wanaouza zana za kilimo,mafundi wa zana za kilimo,wanaotengeneza zana za kilimo,taasisi za fedha na wadau wengine," alisisitiza.
Aliongeza: "Bunifu zitakwenda kwenye mazao manne yamegawiwa katika kanda kuna miradi kulingana na mazao ya eneo mfano Morogoro wanajikita na mbogamboga na alizeti ,Mbeya wana mbogamboga na mpunga, Njombe mbogamboga na mahindi, Singida ni alizeti kila kanda imepewa aina ya zao… tunakwenda kote."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages