A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, April 20, 2024

ORYX, DORIS MOLLEL KUWAONDOA WAUGUZI KATIKA NISHATI ISIYOFAA


Na Mwandishi Wetu 

JUHUDI za serikali kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia zimezidi kuungwa mkono baada ya Kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania kuingia mkataba na Taasisi ya Doris Mollel, kuwapatia mitungi na majiko ya gesi wauguzi kutoka mikoa 10 nchini.


Akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini makubaliano hayo leo Aprili 19, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Kinondoni Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Oryx, Benoite Araman amesema lengo la hatua hiyo ni kutanua matumizi ya nishati ya kupikia katika jamii.


Araman amesema matarajio ya Kampuni hiyo ni kuhakikisha kila Mtanzania anatumia nishati safi ya kupikia.


“Kunahitajika elimu ya kuhakikisha watu wanaokolewa dhidi ya matumizi ya nishati isiyofaa, tunatarajia kutoa majiko mengi zaidi na hadi sasa tumeshatoa majiko 32,000,” amesema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel amesema lengo la kulifikia kundi la wauguzi anya ni kuhakikisha wanawaepusha na athari za matumizi ya nishati chafu ambayo ina madhara kwa jamii.


Doris, ameeleza ugawaji wa majiko hayo utawagusa wauguzi katika mikoa 10.


“Tunatambua nafasi ya wauguzi wa afya, wamekuwa na mchango mkubwa kwenye jamii, tunaona makundi mengine yakipewa majiko sisi tunaona ni muhimu tuwape wauguzi,” ameeleza.


Amebainisha kuwa, majiko hayo yatakabidhiwa kwa wauguzi walio katika mazingira magumu kuwaepusha na matumizi ya nishati yenye madhara 


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Zavery Benela amesema matumizi ya nishati chafu ni moja ya sababu ya magonjwa mengi ya mfumo wa hewa kwa binadamu.


Ameeleza kati ya wagonjwa 500 wa nje wanaopokelewa katika hospitali hiyo, zaidi ya nusu wanasumbuliwa na magonjwa ya mfumo wa hewa.


“Haya ndiyo magonjwa namba moja kwa wagonjwa wengi kwenye hospitali yetu, tumekuwa tukiwapokea na ukiuliza namna anavyoishi utakuta anatumia nishati isiyofaa kupikia,” ameeleza.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Oryx Gas kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.






Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Oryx Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam Dk.Zavery Benela akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakionesha mkataba waliosaini kwaajili ya kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx mmoja wa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini makubalino kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx kwa wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala katika hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala wakifuatilia hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages