Baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha New Faraja kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba pamoja na nasaha kutoka kwa viongozi wa BancABC Tanzania mara baada ya benki hiyo kutoa msaada wa vyakula mbali mbali pamoja na kuwaandalia futari watoto hao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwenye kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadan.
Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa BancABC Tanzania (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula mbali mbali Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto yatima cha New Faraja kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam Ijumaa 29 Marchi 2024 BancABC Tanzania, ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara imetoa msaada wa vyakula mbali mbali pamoja na kuandaa futari kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha New Faraja kilicho Mburahati Jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwenye kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadan.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam mara ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Idara ya Udhibiti BancABC Tanzania Saleh Geva alisema benki hiyo imetoa msaada pamoja na kufuturisha kituo cha Watoto yatima cha New Faraja kama ishara ya kuonyesha upendo pamoja na kuwapa tabasamu na hasa kwenye kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadan. ‘Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanahitaji kuonyesha upendo. Sisi BancABC Tanzania na hasa wafanyakazi tumefarajika sana kujumuika nao pamoja na kupata wasaa wa kufuturu na watoto wanaolelewa kwenye kituo hiki. Kilikuwa ni kipindi faraja sana kwao lakini furaha kwetu kuona watoto hawa wakitabasamu. Lengo letu ilikuwa ni kufanikiwa kuona watoto hawa wajisikia kama sehemu ya Jamii ya Watanzania’, alisema Geva.
Geva aliongeza ‘Kuwafanya watoto hawa watabasamu na kufurai kunawapa matumaini yao ya maisha ya baadae. Kuja kwetu kufuturu na watoto hawa kumetuonyesha kwa nini BancABC Tanzania imekuwa ikijikita sana kwenye kusaidia Jamii ambayo inayotuzunguka. Tutaendelea na utamanduni huu wa kusaidia Jamii ambayo inaishi kwenye mazingira mangumu kwa sababu tunaamini ni moja Kati ya nguzo ya sisi kuendelea kukua kibiashara’,
‘Furaha yetu sisi BancABC Tanzania ni kuona tukibadilisha maisha ya Watanzania. Tunaamini kwenye Jamii yenye usawa na ndio sababu mwaka huu tuliamua kuja kufuturu na watoto hawa ambao wanaishi kwenye mazingira magumu ’, alisema Geva.
‘BancABC Tanzania, ikiwa ni taasisi ya kutoa huduma za kifedha imekuwa ikifanya kazi kubwa sana kuwafikia Watanzania na hasa wale ambao bado hawafikiwa na huduma za kibenki. Kwa sasa, BancABC Tanzania tunao mawakala zaidi ya 700 nchini kote’, alisema Geva huku akiongeza kuwa benki hiyo inayo akaunti maalum kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati kwa ajili ya kutoa mikopo ya kuimarisha biashara zao’.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo cha New Faraja Zamda Idrisa alisema kuwa wamefarijika kwa kuona taasisi binafsi kama BancABC Tanzania ikiunga mkono Jamii ambayo inaishi kwenye mazingira mangumu.
Aliongeza ‘Msaada wenu umekuja kwenye muda muafaka kwani watoto hawa wanahitaji kuonyesha upendo kama watoto wengine. Tunawashukuru kwa msaada wenu na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kuwafungulia riziki kwenye maisha yenu ya kila siku’.
‘Tunatoa rai kwa taasisi zingine pamoja na watu binafsi wazidi kutusaidia kwani watoto hawa wanahitaji kuvaa, kusoma, chakula pamoja na matibabu na kituo chetu hakina wadhamini bali tunatengemea misaada kutoka kwa wadau mbali mbali kama BancABC Tanzania walivyokuja hapa kutusaidia kwa siku ya leo.
No comments:
Post a Comment