Semina ya mafunzo hayo maalum yanaendelea Februari 14-2024 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Flomi Msmavu ambapo uzinduzi wake ulifanywa na Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Bi. Euphrasia Buchuma Februari 13-2024.
Mkurugenzi msaidizi wa USAID Kijana Nahodha, Neemiah Kahakwa, amesema mafunzo hayo ni mafunzo maalum yanalenga kujengeana uwezo waalimu juu ya kuwafundisha Vijana wasiojua kusoma na kuandika.
Neemiah, amesema mradi wa Kijana nahodha ni wa miaka 4 ambapo utekelezaji wake umeanza mwaka 2022 na kumalizika 2024.
Aidha, Neemiah ,amesema mradi huo umejikita katika maeneo 3, ikiwemo kuwapa ujuzi na elimu, kuwapa ujuzi wa kiufundi pamoja na kuwapa elimu ya afya.-
"Mradi wetu ambapo unawalenga vijana kuanzia miaka 15-25 ambao wapo nje ya mfumo wa elimu ambao hawasomi, mradi huu unalenga watu 700 katika Halmashauri zote 3 , lengo kuona hawa vijana wanaelimika wajue kusoma na kuandika kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya Vijana" Amesema Neemiah.
Kwa upande wa Afisa Elimu , Elimu ya Watu wazima Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Emiliana Kishinda, ambaye ni mnufaika wa mafunzo hayo, amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwani Wilaya aliyopo asilimia kubwa ni jamii ya wakulima na wafugaji hivyo asilimia wengi wanakatisha masomo kutokana na kuhama.
Ameshukuru Vijana Nahodha kwa kuja na mradi huo wa mafunzo na wao watahakikisha wanakwenda kuwa sehemu ya hamasa ili kuwafikia Vijana hao kuweza kunufaika na mpango huo.
Halmashauria ambazo zitanufaika na mradi huo ni Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Mvomero.
No comments:
Post a Comment