TAASISI ya WICOF Chini ya Mkurugenzi wake Mwajabu Dhahabu imefanya Kongamano la Mama na Mtoto (Mother and Child outing) likiwa na lengo lakuziba mianya ya vyanzo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Kongamano hilo lemfanyika Ukumbi wa Hotel ya Ottoland iliyopo 88 Manispaa ya Morogoro na kuhudhuriwa na watoa maada mbalimbali ,wazazi pamoja na watoto.
Akizungumza katika Kongamano hilo, Mkurugenzi wa WICOF, na Shule za Green Apple, Mwajabu Dhahabu, amesema semina hiyo ni muendelezo wa program ya malezi ambayo kwa sasa programu hiyo itakuwa inatolewa kwa familia ya watu wachache wachache lengo haswa ni katika kukumbushana juu ya masuala yote yanayohusu malezi na makuzi kwa watoto na kuziba mianya ya vyanzo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Aidha, Bi Mwajabu Dhahabu , amewasisitizia wazazi kuwa karibu na watoto wao hususani katika mipango ya maendeleo kwa kuanzia kwenye ngazi ya familia ili kuleta tija katika ustawi wa familia na taifa Kwa ujumla.
Mwajabu ,amesema kuwa mbinu mbali mbali za wanawake kuepuka utegemezi ni kuwa wabunifu ili kuweza kuzitumia fursa zinazowazunguka na kuhakikisha Kila mwanamke anakuwa na uhuru wa kiuchumi.
Naye mtoa maada na mtalaamu wa masuala ya Jinsia na maendeleo ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof.Fatihiya Massawe, amesema asilimia ya wale wanaofanya matendo ya ulawiti ni wale ambao tayari wameshaathirika na matendo hayo au kwa kuona matendo ya ukatili yanayofanywa mbele yake.
Kwa upande wa Mtaalamu wa malezi na haki za watoto, Dr. Said Simon, amewataka wazazi kuzungumza na watoto wao na kufuatilia mienendo yao kila mara ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili ikiwa pamoja na ubakaji, ulawiti, mimba za utotoni , kuimarisha upatikanaji wa haki na ulinzi wa Mtoto.
Miongoni mwa kazi Mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo mbinu za ustawi wa familia, jinsi ya kutimiza ndoto na malengo, hatua za ujana na madhara yake, kuwa na hofu ya Mungu, madhara ya ukatili wa kijinsia nk.
No comments:
Post a Comment