Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (wa pili kushoto) akipokeza msaada wa msaada wa kabati la kuhifadhia dawa za dharula (Trolley) lenye thamani ya shilingi milioni 2 kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania Ltd, Veronica Chilunda, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
KAMPUNI ya Freight Forwarders Tanzania Limited imekabidhi msaada wa kabati la kuhifadhia dawa za dharula (Trolley) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila lenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Akikabidhi msaada huo Mwakilishi wa Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania, Veronica Chilunda amesema kampuni imeguswa na huduma nzuri zinazotolewa Mloganzila hivyo wameona watoe msaada huo kama sehemu ya kurejesha kwa jamii.
Akipokea msaada huo Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, amewashukuru watumishi wanawake wa kampuni hiyo kwa msaada waliotoa kwani umekuja wakati muafaka wakati hospitali ikiwa katika maboresho hususani katika maeneo ya kutolea huduma na vifaa tiba.
Aidha Bi. Veronica ametoa wito kwa watu na makampuni mbalimbali kujitokeza kusaidia mahitaji katika hospitali hiyo ambayo kwa sasa imepanua wigo wa utoaji huduma.
No comments:
Post a Comment