Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bwana Emmanuel Tutuba (wa pili kulia), akikabidhi tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bwana Isidori Msaki, kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maendeleo ya sekta ya fedha nchini. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na sherehe za kumuaga gavana aliyemaliza muda wake. Prof. florens Luoga (kushoto) na kumkaribisha gavana huyo mpya zilizoandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), mjini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa TBA, Theobald Sabi.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bwana Emmanuel Tutuba (kulia), akikabidhi tuzo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bwana Isidori Msaki, kwa kutambua mchango wake binafsi katika kufanikisha maendeleo ya sekta ya fedha nchini. Hafla hiyo ilifanyika pamoja na sherehe za kumuaga gavana aliyemaliza muda wake. Prof. florens Luoga (wa pili kushoto) na kumkaribisha gavana mpya Bwana Tutuba, zilizoandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), mjini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa TBA, Bwana Theobald Sabi.
BENKI ya Biashara ya DCB imepongezwa kwa mchango wake unaoendelea kuchangia maendekeo ya sekta ya fedha nchini.
Hayo yamebainika katika hafla iliyoandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) katika hafla waliyoiandaa kuzipongeza taasisi za fedha pamoja na kumuaga gavana wa zamani wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga na kumkaribisha Gavana mpya, Bwana Emmanuel Tutuba.
Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Taasisi ya TBA ilikabidhi tuzo mbalimbali kwa benki washirika pamoja na benki ya DCB ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hizo katika Kuhakikisha sekta ya fedha nchini inapiga hatua sawa na malengo ya serikali ya awamu ya sita katika Kuhakikisha watu wengi zaidi wanafikiwa na huduma za kibenki.
Akizungumzia tuzo hizo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bwana Isidori Msaki aliishukuru TBA kwa kutambua mchango wa benki ya DCB na kwake binafsi akisema wanazichukulia tuzo hizo kama deni kwao kwa TBA na kwa wateja wao katika kuhakikisha DCB inaendelea kuwa suluhisho pale watanzania wanapohitaji huduma bora za kibenki.
“Mimi binafsi pamoja na benki yetu tunaona fahari kubwa kupewa tuzo hizi tukizipa umuhimu mkubwa na kuzidi kutuhamasisha kufanya vizuri zaidi katika kuboresha huduma zetu za kibenki ili ziweze kuleta tija na manufaa kwa wateja wetu, wadau na kwa watanzania wote."
“Benki ya DCB itaendelea kuboresha huduma zake na kuongeza bidhaa mpya sokoni zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu, natoa wito kwa watanzania kutumia huduma zetu bora za kibenki na hawatajutia”, alisema Bwana Msaki.
Hii si mara ya kwanza kwa DCB kupewa tuzo ama kutambuliwa kwa mchango wake katika kutoa huduma bora ama kuchangia maendeleo ya sekta za kibenki.
Mwishoni mwa mwaka uliopita, DCB ilitwaa tuzo ya utoaji Huduma Bora za kibenki kwa wateja na pia ilishinda tuzo ya uwasilishaji Bora wa mahesabu zinazotolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA)
No comments:
Post a Comment