Aidha, amesema wana CCM wana kila sababu ya kutembea kifua mbele na majibu kwa wapinzani yapo. Hata hivyo, amempongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, lililodumu kwa zaidi ya miaka 7, tangu mwaka 2015,huku akiwataka Wana CCM hususani upande Jumuiya ya Vijana kuanza kupambana majukwaani kumsemea Mhe. Rais na Serikali yake kwa yale anayoyafanya ya kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuwajibu wapinzani kwa hoja na sio vurugu.
"Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesharuhusu mikutano ya hadhara , kikubwa tujipange sasa na tuwe na taarifa za uhakika za miradi ambayo Mhe. Rais anaifanya tukiwa na Data nzuri hii ndio itakuwa silaha yetu kwa wapinzani na kukifanya Chama chetu kuendelea kushika Dola haswa tukianza mwaka 2024 ambapo tutakabiliwa na uchaguzi wa Wenyeviti wa Mitaa na 2025 uchaguzi Mkuu" Amesema Mhe. Mzeru.
" Niwakumbushe kuwa uwepo wa Tawi hili hapa chuo ni sehemu ya kuwapika viongozi , wapo viongozi wengi wamepikwa hapa na wengine mmewataja kama vile Naibu Waziri, Mhe. Hussen Bashe waziri, Mhe. Antony Mtaka Mkuu wa mkoa, Mhe. Nape Moses Nauye Waziri, Mhe. Mama Anna Makinda spika wa bunge mstaafu, pamoja na viongozi wengine wa serikali na chama katika Taifa letu" Ameongeza Mhe. Mzeru. Amesema kuwa huu ni muda sasa wa Wana CCM kufanya siasa za kistaarabu, siasa za kupevuka, siasa za kujenga sio za kubomoa, si kurudi nyuma kwani hapa taifa lilipofikia lipo katika Aamani kubwa na chama cha CCM kinaamini katika kukosolewa na kujikosoa. Pia, Mhe.
Mzeru, amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kufanya yale yaliyowapeleka chuoni hapo ili waweze kutimiza ndoto zao. Mbali na Ugawaji wa Kadi, pia aligawa Seti ya Jezi kwa upande wa mpira wa miguu pamoja na mpira mmoja huku upande wa Netball akitoa jezi na mpira wake kwa ajili ya kuimarisha michezo kwa Jumuiya hiyo. Mwisho, amewaahidi kukarabati Ofisi ya Tawi hilo Maalum kutokana na changamoto ya uchakavu wa Ofisi hiyo.
No comments:
Post a Comment