Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Bw. Imani Kajula akizunguza na wanasimba kwenye mkutano mkuu wa Uchaguzi unaofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC Posta jijini Dar es Salaam.
………………………………………………..
Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Bw. Imani Kajula amesema yeye siyo CEO, ila ni CCO, kazi yake ni kuwaunganisha wanasimba wote ili kuwa kitu kimoja Ningependa muichukulie kazi yangu kuwa kiunganishi kwa wote kuliko kuwa kiongozi zaidi.
“Kwa namna ya kipekee nimshukuru sana aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba Barbra Gonzalez kwa moyo wake, jana alinipigia simu, kesho tutaongea na Jumatano ijayo tutakutana ili kuwa na mwendelezo mzuri kwa amendeleo ya Simba Sports Club.” Amesema Imani Kajula.
Ameongeza kuwa wanachama ndiyo roho ya Simba , bila ninyi hakuna Simba. Cha kwanza ni kuhakikisha tunaboresha mawasiliano, kuhakikisha tunawasikiliza ili katika maendeleo yetu ya Simba twende pamoja.
Ametanabaisha kwamba ataimarisha matawi, sana, “utajengwa mfumo endelevu ili miaka ijayo tufanye mkutano wa kiteknolojia kwa kushirikisha watu wote nchi nzima.”
“Tunataka tushinde, lazima kujenga timu bora lakini kazi ya pili ni kujenga taasisi imara na endelevu hata nisipokuwepo kuwe na mtu mwingine wa kuendeleza. Lakini pia kujenga chapa imara, tunayo lakini kuongezea mapato.” Amesema Imani Kajula
Akizungumzia Ligi ya Mabingwa Afrika kajula amesema Kwenye Ligi ya Mabingwa (wanaume) tunataka kufanya vizuri zaidi kwa sababu timu yetu ya wanawake imefanya vizuri sana Afrika hivyo hatuna budi kuhakikisha timu ya wanaume inafanya vizuri zaidi ni lazima tuongeze wadhamini wengine moja ya kazi yangu sasa ni kwenda kuwatembelea wadhamini wetu na kutafuta wadhamini zaidi.
“Lengo la timu yetu ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, lakini Ligi ya Mabingwa Afrika kufika robo fainali au zaidi. Simba SC kufanya vizuri zaidi Afrika na kuboresha timu za vijana.”-amesema Imani Kajula.
Credit – Fullshangwe Blog.
No comments:
Post a Comment