Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (katikati) akikata keki huku wafanyakazi na wateja wa Benki ya tawi la Victoria wakishangilia, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.
Benki ya Biashara ya DCB imeendelea kung'ara wakati ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu huku ikianisha baadhi ya mafanikio iliyopata tangu ilipoanzishwa Mwaka 2000.
- Benki ya kwanza kufuzu kutoka benki ya kijamii kwenda Benki ya Biashara.
- Benki ya kwanza Tanzania kusajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
- Benki inayoongozwa na watanzania kuanzia Bodi ya Wakurugenzi hadi Menejimenti.
- Benki imewanyanyua wajasiriamali wanawake zaidi ya 400,000 kupitia mikopo ya vikundi.
- Benki inatoa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja.
- Benki ina Wateja kuanzia wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, wateja binafsi, waajiriwa, mashirika na makampuni.
- Benki ipo sambamba na waajiriwa na inatoa mikopo yenye riba nafuu.
- Benki ipo sambamba na wazazi kuwawezesha watoto elimu hadi chuo kikuu kupitia akaunti ya Skonga na mkopo wa ada.
- Benki inatoa mikopo ya nyumba yenye masharti nafuu.
- Fanya miamala na malipo mahali popote kupitia DCB Pesa, DCB Wakala, Visa, Master Card QR, DCB Malipo na Internet Banking.
- Kufanya miamala nje ya nchi kupitia International money transfer na Western Union.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa pili kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa mmoja wa Wateja wa Tawi la DCB Victoria, Halima Iddi, katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo tawini hapo, jijini Dar es Salaam wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya DCB, Nelson Swai (katikati), akikabidhi msaada wa viti, mashine ya kuchapia (printa) na mifuniko ya tairi za gari vilivyotolewa na DCB kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Magomeni, Mrakibu wa Polisi Edward Masunga, ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kituoni hapo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Beki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki katika moja ya shamrashamra wakiwapokea Wateja wao wajasiriamali wa mikopo ya vikundi waliofika katika hafla ya kuwapongeza katika makao makuu ya benki hiyo, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza na wajasiriamali ambao kutoka vituo mbalimbali ambao ni wanufaika wa mikopo ya vikundi inayotokewa na DCB. Katika hafla hiyo DCB ilivitambua vituo bora na kukabidhi vyeti vya shukurani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii.
No comments:
Post a Comment