A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, September 21, 2022

TADB Yaibuka Mshindi Wa Pili Mifuko Na Programu Za Uwezeshaji

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) akimpa mkono wa pongezi Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Mzee Kilele  baada ya TADB kupata tuzo ya mshindi wa pili kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima wadogo (SCGS) katika kundi la "Mifuko na Programu za Uwezeshaji". Tuzo hizo zimetolewa katika Kongamano la Sita (6) la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi - NEEC jijini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Mzee Kilele akipokea Tuzo kutoka kwa Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb) baada ya TADB kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima wadogo (SCGS) kuwa Mshindi wa pili katika kundi la "Mifuko na Programu za Uwezeshaji". Tuzo hizo zimetolewa katika Kongamano la Sita (6) la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi - NEEC  jijini Dodoma.

 Meneja msimamizi wa Mfumo wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) kutoka TADB Bi. Asha Tarimo akionesha Tuzo baada ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima wadogo (SCGS) kuwa Mshindi wa pili katika kundi la "Mifuko na Programu za Uwezeshaji". Tuzo zilizotolewa katika Kongamano la Sita (6) la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi - NEEC jijini Dodoma. Hadi sasa TADB kupitia Mfuko huo umeshatoa zaidi ya Bilioni 150 kwa wakulima wadogo nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages