NA MWANDISHI
WETU
JUMUIYA
ya Wazazi Tanzania
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , imekemea vikali vijana wanaojihusisha na
vitendo vya uhalifu wanaojiita Panya Road na kuzitaka mamlaka kuchukua hatua
kali dhidi yao.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Dar es Salaam, leo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo , Dk.
Edmund Mdondwa, amesema kuibuka kwa wahalifu hao kunachangiwa na mmomonyoko wa
maadili katika jamii hasa wazazi kushindwa kusimamia vema malezi.
Dk. Mndolwa
amesema, ugumu wa maisha siyo
kigezo cha wahalifu hao
kujiingiza katika vitendo hivyo kwani
kama shida yao ingekuwa ni kuiba mali wasingekuwa wanaua watu wasio na
hatia.
Ameeleza ili kukomesha
vitendo hivyo hasa kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 18
ni vyema hatua kali zikachukuliwa kwa
mhalifu na mzazi wake.
“Kama
mhalifu analala ndani na wazazi
wake lakini usiku anamka kwenda kuua
watu na kurudi basi ni lazima yeye na
mzazi wake wawajibishwe,”amesemaa Dk. Mndolwa.
Pia ameshauri
Bunge la Jamhuru ya Muungano wa Tanzania
kuangalia mabadiliko ya sheria itakayo wabana wahalifu wenye umri wa chini ya miaka 18 wanaojihusisha
katika uhalifu huo.
“Jambo la
kusikitisha Panya Road wengi wana umri wa
chini ya miaka 18 hivyo watahukumiwa kwa sheria za watoto. Kuna
umuhimu wa kubadili sheria hizi kwa kuwafunga wahalifu wanaojihusisha na matukio
hayo ya kuua watu,”ameeleza sha Dk. Mndolwa.
Amebainisha kama
wahalifu hao watahukumiwa hata kwa sheria za watoto basi wafungwe katika
magereza maalumu za watoto .
Dk. Mndolwa
amesema ili kukabiliana na matukio kama hayo ni vyema serikali kuchukua
hatua hasa kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kwa kufanya marekebisho ya mitaala ya elimu ili elimu
inayotolewe imsaidie mtoto kujiajiri.
“Pia somo
la dini lirejeshwe shuleni na elimu
ya maadili, utamaduni, uzalendo na wazazi wawe chachu ya kuwapa malezi bora
watoto wao hali itakayo punguza kasi ya vijana kujiingiza katika matukio hayo
ya kihalifu,”amesema.
Hivi
karibuni vitendo vya kihalifu vimeibuka
katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, vinavyodaiwa kutekelezwa na
kundi la Panya Road na kusababisha hofu kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment