Waziri
wa Katiba na Sheria George Simbachawene akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Taasisi Mafunzo ya
Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo Machi 10, 2022 Dar es
Salaam.
Makamu
Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Machapisho, Law Shool Profesa Zakayo
Lukumay akieleza jambo mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria George
Simbachawene pamoja Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud mara baada
ya waziri huyobn kumaliza kufanya ziara kwenye taasisi hiyo leo Machi
10, 2022 Dar es Salaam.
Baadhi
ya watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini
(Law School) wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria George
Simbachawene baada yanm kumaliza kufanya ziara yake kwenye taasisi hiyo
leo Machi 10 2022 Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Geofrey Pinda aliyesimama akizungumza
na watumishi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheri kwa Vitendo baada ya
Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene kumaliza kufanya ziara
kwenye Taasisi ya hiyo leo Machi 10, 2022 Dar es Salaam
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe.George Simbachawene akipokelewa na Mkuu wa
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) Dkt.
Benhajj Masoud pamoja na watumishi wa taasisi hiyo kufanya ziara kwenye
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo nchini (Law School) leo
tarehe Machi 10, 2022 Dar es Salaam.
WAZIRI
wa Katiba na Sheria George Simbachawane amevushauri vyuo
vinavyofundisha taaluma ya sheria nchini kuhakikisha wanaweka vitengo
vya kutoa msaada wa huduma ya kisheria kwa wananchi wote hasa wale
wasiokuwa na uwezo ili kupeleka haki mbele
kama ambavyo shule ya sheria nchini inatoa huduma hiyo.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo Machi 10 2022, wakati wa ziara yake katika Chuo cha sheria Dar es Salaam.
Amesema
kuwa huduma ya msaada wa sheria ipo kwa mujibu wa sheria na kwamba
Serikali imeanzisha kitengo hicho " Ofisini kwetu yupo Mkurugenzi
anayeshughulika na huduma na anasajili watoa huduma hiyo na wizara hiyo
inahakikisha kila mwananchi anapata haki yake
"Nchi
yetu bado inahitaji wanasheria ama mawakili ili kusaidia wananchi na
Taifa kwa ujumla na ndio maana hivi karibuni serikali imetunga sheria ya
msaada wa kisheria ambao unatolewa bure na Taasisi, watu mbali mbali na
wizarani ambako kuna mkurugenzi anayehusika na usajili ya huduma hiyo
ya msaada wa kisheria ambae pia anawasajili watoa huduma.
"Nakipongeza
Chuo hiki kwa kuwa na utaratibu mzuri kwani nimekuta wamefungua kitengo
cha msaada wa kisheria na wanatoa huduma hii bure" amesema
Simbachawene.
Amesema,
amefurahi sana kuona namna wanafunzi wa Chuo hicho wanavyoandaliwa
kwenda kutatua changamoto mbali mbali za kisheria kwa wananchi na Taifa
kwa ujumla .
Aidha
nakipongeza sana Chuo hiki na uongozi mzima kwa kufanikisha ile kazi
ambayo serikali ilikusudia ya kuandaa mawakili ili waweze kuwa na uwezo
wa kushindana na mawakili wengine dunia na wamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa.
"
Saizi dunia inaishi kwenye mitandao katika makubaliano, unapokuwa na
wanasheria wazawa ambao wameiva vizuri unakuwa umetengeneza silaha kubwa
katika nchi kama vile tunavyoweza kununua silaha za kijeshi katika
kulinda nchi", amesema Simbachawene
Aidha
Simbachawene amesema, Chuo cha sheria kinaandaa watu kwenda kufanya
uwakili na siyo mwanafunzi kufaulu mtihani, kwa hiyo ule uwezo ambao
mwanafunzi atakuwa ameupata kuweza kumsaidia mteja wake kwa vitendo
ndio utakaomuwezesha kufaulu vizuri.
Amesema,
uwakili ni kuongea siyo kuandika hivyo kama wakiingia Chuo wanafunzi
mia nane na wakatoka mia mbili sisi tunaamini kuwa Chuo kinafanya kazi
nzuri kwa hawa wanasheria wanaotaka hapa wanaenda kusimamia viapo,
mikataba kuandaa kuunganisha watu na kusuluhisha mambo mbalimbali.
"
Hakuna maneno maneno kwenye taaluma ya sheria kama maeneo mengine,
hivyo hatuwezi kuchukua kama mtihani wa shule au vyuo vya kawaida ili
wanafunzi watoke tu, hapana ikifanyika hivyo tutakuwa tumearibu maana
nzima ya kuwajengea uwezo wanafunzi hawa ili tuweze kuwa na mawakili
wazuri katika Kanda na dunia kwa ujumla.
Aidha
amesema, Chuo kinahitaji kuwa na vitendea kazi vya kisasa, ili hatimae
nao waweze kwenda sambamba na Mhimili wa Mahakama ambao kwa sasa umefika
mbali katika masuala ya ICT kwabi sasa unaweza pata huduma za Utabiri
kimahakama kutokea mahali popote kwa njia ya mtandao.
Naye,
Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Benhajj Masoud amesema wamefarijika na ziara
ya Waziri huyo chuoni hapo kwa kuwa imewaongezea hamasa katika masuala
mbalimbali na kwamba wataendelea kutimiza majukumu yao hasa katika
kuhakikisha wahitimu wanaotoka mahali hapo wanakuwa na weledi wa
kutosha.
No comments:
Post a Comment