KAMATI ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Tume ya
Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa hatua iliyofikia katika utekelezaji
wa Ujenzi wa Maabara Changamana Awamu ya Pili.
Kamati
hiyo Machi 15, 2022 ilifanya ziara Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za
Atomiki Tanzania (TAEC) ili kukagua maendeleo ya mradi huo wa ujenzi wa
Maabara Changamana Awamu ya Pili.
Katika
ziara hiyo, Kamati ya Bunge iliipongeza TAEC kwa hatua kubwa iliyofikia
katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Serikali kwa
jumla ya kiasi cha shilingi Billioni 10.4.
Akitoa
taarifa ya mradi kwa Kamati ya Bunge Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa
Lazaro Busagala alisema awali TAEC iliingia mkataba na Wakala wa Ujenzi
Tanzania (TBA) kwa ajili ya ujenzi wa maabara awamu ya kwanza Mei 29,
2017.
Ujenzi
rasmi wa Maabara Changamano awamu ya kwanza uliaanza Juni Mosi, 2017,
ambapo ulikamilika kwa kiasi cha shilingi billioni 2.3 na kuzinduliwa
rasmi na Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania tarehe 29 Aprili 2018.
Ujenzi
wa Maabara ya Awamu ya pili unahusisha Maabara zifuatazo; i. Maabara ya
kupima mionzi ya Alpha (Alpha Spectrometry Laboratory); ii. Maabara ya
kupima mionzi ya Beta (Beta Counting Laboratory); ya kupima mionzi ya
Gamma (Gamma Spectrometry Laboratory); iii. Maabara ya kupima mionzi
kwenye damu (Cytogenetic Laboratory);
iv.
Maabara ya kupima viwango vya metali kwenye sampuli (X-Ray Fluorescence
Laboratory); 4 v. Maabara ya kufanya matengenezo ya vifaa vya mionzi
(Nuclear Instrumentation and Maintanance Laboratory); vi. Maabara ya
uandaaji wa sampuli kikemikali (Radiochemistry Laboratory); vii. Maabara
ya kufanyia matengenezo mabaki ya vyanzo vya mionzi (Radioactive Wastes
Conditioning Laboratory).
Profesa
Busagala alisema kuwa, hadi kufikia Machi 9, 2022, hatua iliyofikiwa ya
ujenzi wa Maabara Changamana Awamu ya Pili (mradi namba 6352) ujenzi
ulikuwa umefikia asilimia 94 ambapo upo mbele kwa miezi mitatu
ukilinganisha na mpango kazi (work program) uliokuwa umepangwa kwenye
mkataba.
Akimalizia
taarifa yake Profesa Lazaro aliishukuru Kamati ya Bunge na kutoa
shukrani za dhati kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kwa kuendelea kuisimamia, kuitegemeza na kuiwezesha TAEC
katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiiomba Serikali
iendelea kuiwezesha taasisi kufikia malengo yake kwa manufaa ya jamii ya
Watanzania.
No comments:
Post a Comment