CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku,28, yuko tayari kukatwa mshahara kwa ajili ya mchakato wa kurejea Inter Milan kwa mkopo (Calciomercato in Italian)
Lukaku amekasirishwa na madai kuwa anajaribu kutumia vibaya hali ya Chelsea na kuwa hana nia ya kuondoka katika klabu hiyo. (Telegraph )
Juventus wanalenga kuwanunua wachezaji wawili wa kimataifa wa Italia wa Chelsea - kiungo Jorginho, 30, na beki wa kushoto Emerson Palmieri, 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Lyon. (Tuttosport - in Italian)
Barcelona pia wanaifuatilia Chelsea na wanavutiwa na wachezaji wao wawili wa kimataifa wa Uhispania - mlinzi wa kushoto Marcos Alonso, 31, na mlinzi wa kulia Cesar Azpilicueta, 32, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu. (Mundo Deportivo)
Ombi la Saudi Media la kutaka kuinunua Chelsea ni pamoja na mipango ya kuunda upya Stamford Bridge na kuwaongezea kandarasi wachezaji kama vile Azpilicueta na mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 29, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kuisha msimu huu wa joto. (Goal)
Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 29, anataka kusalia kwenye Ligi ya Primia ikiwa hatakubali kusaini mkataba mpya na Liverpool. (Football Insider)
CHANZO CHA PICHA,PA MEDIA
Manchester United wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad na Uswidi Alexander Isak, 22. (Star)
Mkufunzi binafsi wa Paul Pogba anasema kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 28, ataondoka Manchester United mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato)
Newcastle wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu. Mchezaji huyo 24, mkataba wake unamalizika msimu wa joto (Times)
Manchester United wanaweza kuchukua hatua ya kumrejesha Sam Johnstone kutoka West Brom msimu wa joto, ingawa Tottenham na Southampton pia wana nia ya kumsajili mlinda mlango huyo wa England mwenye umri wa miaka 28, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru. (Sun)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Chelsea watamsajili kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 27, kutoka Atletico Madrid msimu huu - ikiwa vikwazo vya serikali ya Uingereza vitawaruhusu. (Mirror)
Chelsea imeiomba serikali ya Uingereza kuondoa marufuku ya kuwaongezea mikataba wachezaji huku kukiwa na hofu kuwa huenda ikawaacha na mzozo mkubwa wa ulinzi msimu ujao. (Telegraph )
Manchester United wamejulishwa kuhusu uwezekano wa kocha wa Chelsea Thomas Tuchel kupatikana mwishoni mwa msimu huu. (Mail)
Kocha wa Ajax Erik ten Hag yuko tayari kuwa kocha wa Manchester United - na yuko tayari kuwa pamoja na kocha wa muda Ralf Rangnick kwenye benchi. (Mirror)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Real Madrid wanataka kumbakisha kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru kwa angalau msimu mwingine lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 bado hajasaini mkataba mpya. (Marca- in Spanish)
AC Milan wamefikia makubaliano na Lille kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Renato Sanches, 24, msimu wa joto. (Calciomercato - in Italian)
Juan Mata anaweza kupewa nafasi ya ukocha katika klabu ya Manchester United - ikiwa kiungo huyo wa kati wa Uhispania, 33, atastaafu mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (Sun
No comments:
Post a Comment