A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 14, 2022

Spika Tulia Awatembelea Prof. Jay na Mama wa Halima Mdee

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), leo Machi 14, 2022 amewatembelea na kuwajulia hali Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay pamoja na Mama mzazi wa Mbunge wa viti maalum CHADEMA, Mhe. Halima Mdee, Bi. Theresia Mdee, ambao wamelazwa na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya taifa Muhimbili iliyopo Jijini Dar es salaam.

Dkt. Tulia ameelezwa kuwa hali za wagonjwa hao zinaendelea kuimarika kila siku tofauti na awali ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wahudumu wa hospitali hiyo wakiwemo Madaktari ambao wamekuwa wakijitolea kwa nguvu zote katika kuokoa maisha ya watu.

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kuwa vyombo vya dola vinafanya uchunguzi kubaini aliyemrekodi Prof. Jay (ICU). Ameagiza Hospitali zote nchini kuweka matangazo yanayokataza kupiga picha bila kibali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages