A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, March 6, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA CRDB JIJINI DAR ES SALAAM

1-7-1024x950 2-7-1024x617
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela pamoja na viongozi wengine Wakuu wa CRDB pamoja na Serikali akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Palm Beach, Mkabala na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
3-3-1024x787 4-1024x814 5-2-1024x814
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wengine Wakuu wa CRDB pamoja na Serikali akiminya kitufe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Benki ya CRDB lililopo Palm Beach, Mkabala na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
6-1-1024x665 9-2-1024x926
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela wakati akikagua Ofisi mbalimbali za Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo pembezoni mwa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
7-2-1024x756 8-2-1024x951
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB pamoja na viongozi wengine wa Serikali katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo pembezoni mwa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
13-1024x530 14-1-1024x534 15-1024x539 16-1024x539 17-1024x560
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa CRDB mara baada ya kuzindua jengo la Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo pembezoni mwa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
12-1-1024x804 20-1024x602
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiagana na viongozi mbalimbali wa Benki ya CRDB mara baada ya kuzungumza nao katika viwanja vya Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania | Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema uwepo wa sekta ya kibenki iliyo imara nchini huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira na kutoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato.

Rais Samia amesema hayo katika Hafla ya Uzinduzi wa Makao Makuu ya Benki ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema benki ya CRDB imefanya vizuri katika kutoa fursa za ajira, biashara na ujasiriamali kwa sekta binafsi wakiwemo bodaboda, mama lishe na wamachinga.

Aidha, Rais Samia ameitaka benki hiyo kuendelea kuyawezesha makundi hayo ili kutayarisha walipa kodi na kutanua wigo wa Serikali kukusanya mapato kupitia makundi hayo.

Rais Samia pia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kifedha huku akiongeza kuwa sekta za kibenki zina jukumu la kufufua uchumi uliodorora kutokana na UVIKO 19.

Serikali kupitia Benki Kuu imeanzisha mpango mahsusi wa kuiwezesha sekta ya kibenki kupata mikopo yenye riba nafuu ambapo imetenga jumla ya shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuyakopesha mabenki kwa masharti nafuu zitakazowezesha kuikopesha sekta binafsi nchini.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages