Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MBUNGE
wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba ametimiza ahadi yake ya
kutoa msaada kwa Binti mwenye ulemavu, Loyce Peter aliyeomba msaada huo
wakati wa maandalizi ya pambano la masumbwi kati ya Bondia Abdallah Pazi
(Dullah Mbabe) dhidi ya Twaha Kassim Kiduku.
Akizungumza
wakati akikabidhi Msaada huo wa Pikipiki aina ya ‘Boxer’ kwa Binti
huyo, Mhe. Tarimba amesema alikutana na Loyce wakati wa maandalizi ya
pambano hilo, Agosti, 2021. Amesema alitoa ahadi ya kununua Bajaji
lakini kutokana na mahitaji ya Jimbo (Kinondoni) imeshindikana kununua
Bajaji na kushauri kununua Pikipiki.
“Lengo
ilikuwa kununua Bajaji lakini kutokana na mahitaji mengi ya Jimbo,
niliomba mbele ya familia yao, bora tununue Pikipiki ili imsaidie yeye
na familia yake kupata riziki ya kila siku”, amesema Mhe. Tarimba.
Kwa
upande wa Binti huyo, Loyce Peter ameshukuru Mhe. Bunge wa Kinondoni
kumpatia msaada huo aliomuahidia mwaka jana walipokutana katika Jimbo
hilo.
“Mungu
akubariki, akuongezee na pia usichoke kutusaidia sisi wenye uhitaji
maalum, ukitoa japo kidogo, Mungu atakuzidishia kile ulichotoa. Mimi
nishakuwa mwanao, umenisaidia mimi umesaidia wengi, mimi nitasadia
wengine. Ahsante!”, ameeleza Loyce.
Naye,
Mama Mzazi wa Loyce, Bi. Restuta Paulo Mbyalu amemshukuru Mbunge
Tarimba kutimiza ahadi hiyo aliyowaahidi kuwapatia msaada huo. Pia
amemuomba kusaidia wengine wenye uhitaji kama alivyosaidiwa yeye kwa
Mtoto wake Loyce.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Haroud Maruma
amempongeza Mbunge Tarimba kutimiza ahadi hiyo kwa Binti huyo mwenye
ulemavu. Amesema amefanya jambo hilo la kiungwana na la ki Mungu.
“Nitoe
rai kwa Viongozi, Wilaya ya Kinondoni bado watu wengi wana nahitaji,
asiwe Mbunge pekee, bali wengine watoe misaada kwa Wananchi wenye
mahitaji, kwa sababu jambo hili ni la kiungwa na la ki Mungu”, amesema
Maruma.
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba (wa kulia) akikabidhi
Pikipiki kwa binti mwenye ulemavu, Loyce Peter. Mhe. Tarimba amekabidhi
Pikipiki hiyo baada ya kutoa ahadi mwaka jana.
Mama
Mzazi wa Loyce Peter akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Mtoto
wake kukabidhiwa Pikipiki na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM), Mhe.
Abbas Tarimba.
ulemavu,
Loyce Peter (wa kushoto) akizungumza baada ya kukabidhiwa Pikipiki hiyo
aliyoahidiwa na Mbunge wa Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba.
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Mhe. Abbas Tarimba akizungumza na Waandishi
wa Habari wakati akikabidhi msaada wa Pikipiki kwa binti mwenye
ulemavu, Loyce Peter, tukio la kukabidhi ahadi hiyo limefanyika katika
Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
Mwenyekiti
wa CCM, Wilaya ya Kinondoni, Haroud Maruma akizungumza wakati Mbunge wa
Jimbo hilo akikabidhi msaada wa Pikipiki kwa binti mwenye ulemavu,
Loyce Peter.
No comments:
New comments are not allowed.