Kilimo kimekuwa uti wa mgogo wa uchumi wa Tanzania tangu uhuru, ambapo kinaajiri na kutoa mchango mkubwa kwa Pato Ghafi la Taifa. Kwa kuzingatia suala hili, KILIFAIR Promotion, taasisi inayoongoza katika kuandaa maonesho ya biashara ya kimataifa nchini, inazindua maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatakayojulikana kama “TANZFOOD Expo”, yatakayofanyika katika Viwanja vya Magereza, Arusha kuanzia Ijumaa ya tarehe 11 Machi hadi Jumapili ya tarehe 13, ambapo maonesho yatakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 11 kila siku.
Hafla
ya ufunguzi wa TANZFOOD itazinduliwa rasmi na Waziri wa Kilimo, Mh.
Hussein Bashe pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi. Regine
Hess saa 5 asubuhi siku ya Ijumaa ya tarehe 11 Machi. Wageni wengine
maalumu katika maonesho hayo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt.
John Mongella.
Maonesho
hayo yatawaleta pamoja zaidi ya makampuni 120 kutoka Tanzania na nchi
jirani za Afrika Mashariki. Maonesho hayo yatashirikiana na Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), GIZ, TAHA na wadau wengine muhimu wenye dhamira
ya kuendeleza sekta ya Kilimo nchini Tanzania.
“Tunaelewa
kwamba sekta hii si tu kwa ajili ya Taifa letu la Tanzania bali
inalisha nchi nyingine nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hii ndiyo
sababu tuliamua kuwekeza katika maonesho yenye viwango vya kimataifa ili
kwamba tujivunie vya kutosha na kuonesha “Ladha ya Tanzania” kama
kibwagiz cha maonesho huyo kinavyosema,” alisema Dominic Shoo, mmoja wa
Wakurugenzi wa KILIFAIR Promotion.
“Na
sisi tunafurahi kuona mwitikio wa waoneshaji kutoka ndani ya Tanzania
na masoko mengine. Maonesho haya si tu yataonesha bidhaa, bali itawaleta
wataalamu mbalimbali wa Sekta ya Kilimo ili kutoa ujuzi wao kamilifu
kwa makampuni yanayoshiriki na wakulima watakaofika katika maonesho
haya,” alisema Mkurugenzi wa KILIFAIR Tom Kunkler, akiongeza:
“Tumeanzisha Semina na Warsha ili kuwaelimisha wakulima kuhusu kuongeza
ubora na maendeleo katika sekta hii.”
Tukio
hili la siku tatu litagawanyika katika siku za wanafanya biashara (B2B)
ambayo itakuwa Ijumaa na kwa kiasi fulani Jumamosi na siku za
watumiaji/familia katika siku za Jumamosi na Jumapili. Katika kipindi
chote hiki, wageni watatumia kujenga mtandao wa kibiashara katika
mazingira rafiki ya kitaalamu, kufurahia burudani kutoka kwa wasanii wa
hapa nchini na aina anuwai za vyakula vya kitanzania.
Bw.
Antony Chamanga, Meneja Mkuu wa Maendeleo wa TAHA alieleza furaha yao
kuwa sehemu ya maonesho kama hayo yanayoonesha hali ya ubora na ladha ya
vyakula vya Kitanzania. “Sisi tuna wakulima 19,700 ambao ni wanachama
wa TAHA na wanazalisha bidhaa za mbogamboga zenye ubora wa juu
zinazokidhi viwango vya masoko ya kimataifa. Kwa hiyo, tunafurahi kwamba
wanachama wetu watakaohudhudia maonesho haya, watoana fursa tele
zilizopo katika sekta ya kilimo na jinsi gani ushiriki wao katika setka
hii unavyoweza kusaidia kupeperusha bendera ya Taifa katika masoko ya
kimataifa,” alisema Antony.
Miongoni
mwa washirika na wadhamini wengine wa maonesho haya ni Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) na GIZ ambao wamewekeza kiasi kikubwa sana katika
kuwajengea uwezo wakulima wa hapa nchini na wadau wengine wa kilimo kwa
kuwapatia fursa rahisi katika sekta hiyo kupitia upatikanaji wa fedha
zinazohitajika ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali za kilimo.
Mdhamini
mwingine wa kimkakati ni Benki ya CRDB, ambayo imekuwa na dhamira ya
dhati kuhakikisha wakulima wadogo wanapata msaada wa kifedha na
kujumuishwa, ambavyo wanahitaji vyote hivi ili kuchangia katika kuleta
usalama wa chakula na kuimarisha ubora wa maisha ya Watanzania.
Wadhamini wengine ni pamoja na Bakhresa Group (AZAM), Coca Cola, Pepsi
Cola, BLINK WIFI na kundi la HARSHO miongoni mwa makampuni mengi
maarufu.
Maonesho
haya ya kila mwaka yatawaleta pamoja wadau wa kilimo wanaotoka katika
sekta mbalimbali zinazohusiana na kilimo na kuangazia maeneo mbalimbal
kwa ubunifu katika kilimo, ufungashaji na usindikaji, mbegu bora,
pembejeo za kilimo, viuatilifu na kemikali. Vilevile kutakuwa na maeneo
maalumu kwa ajili ya semina & warsha ili kutoa elimu na kuongeza
ujuzi kwa wakulima katika siku hizo zote tatu za maonesho. Na tukio hilo
pia litarushwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari,
vituo vya runinga, redio na kurasa rasmi za kijamii za TANZFOOD Expo.
No comments:
Post a Comment