A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 10, 2022

GF Trucks & Equipment’s Ltd Yasaini Mkataba Kusambaza Vifaa Miradi Ya Maji

 

.com/img/a/
Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks Equipment’s Ltd, Imran Karmali (kulia) na Katibu mkuu Wizara ya maji Eng Anthon Sanga wakisaini mkataba wa kusambaza vifaa kwa ajili ya miradi ya maji uliofanyika jijini Dodoma. Picha na Said Khamis.
.com/img/a/
.com/img/a/
Mkurugenzi wa Bing Bang akibadilishana nyaraka na Katibu mkuu Wizara ya maji Eng Anthon Sanga wakati wa hafla ya kusainin mikatyaba na makampuni ya kusuply vifaa katika miradi ya maji nchini.
.com/img/a/
.com/img/a/
Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks Equipment’s Ltd ,Imran Karmali(kulia) na Katibu mkuu Wizara ya maji Eng Anthon Sanga wakionesha mikataba baada ya kusaini kwa ajili ya kusambaza vifaa vya miradi ya maji mipya nchini wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dodoma. Picha na Said Khamis

Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd Imeingia mkataba na serilkali wa kusambaza vifaa vya miradi ya maji ikiwa ni jitihada za serikali kuhakikisha inamaliza tatizo la maji mijini na vijijini.

Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo Katibu mkuu Wizara ya Maji nchini Mhandisi Anthon Sanga aliwataka walioshinda tenda hizo za 'kusuply' vifaa hivyo kuhakikisha wanakamilisha na kukabidhi kwa wakati na isizidi mwezi wa tano ili kuendana na kasi ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha miradi inamalizika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugezi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd Imrani Karmali alisema wao wamelipokea agizo hilo la kukamilisha na kukabidhi vifaa hivyo kwa wakati.

Pia aliishukuru Serikali kwa kuaminiwa na kwamba wao kama Kampuni hawataingusha katika hilo na ikiwezekana kabla ya mwezi wa tano kila kitu kitakuwa tayari,Ikizingatiwa kuwa GF inayomiliki kiwanda cha kutengeneza Magari hapa hapa nchini Tanzani kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Mwisho kupitia miradi ya maji wao itakuwa kazi nyepesi kwao kwani kupata kwa tenda hiyo kutaongeza Tija katika kiwanda chao na kwa kuwa wana wataalamu wa Kitanzania itakuwa rahis kukamilisha mahitaji kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages