A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 5, 2022

PETER BANDA AONDOKA SIMBA SC


Na: Stella Kessy.


Winga peter banda ameondoka leo kuelekea Malawi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afcon inayofanyika nchini Cameroon kuanzia january 9.

Banda amekwenda moja kwa moja Cameroon ambapo atakutana na Wachezaji wenzake tayari kwa Mashindano hayo.

Hata hivyo Malawi imepangwa kundi B pamoja na timu Senegal, Zimbabwe na Guinea, the flames itaanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya Guinea januari 10.

Banda amefurahi kushiri katika michuano hiyo kwa kuwa atakutana na Wachezaji wakubwa wanaofanya vizuri barani Ulaya ambapo atajifunza mengi kutoka kwao.

Ameongeza kuwa atahakiksha anafanya vizuri ili kulisaidia taifa lake na kuitangaza Simba kupitia michuani hiyo mikubwa barani Afrika.

"Hii ni michuano mikubwa na kila mchezaji afrika anatamani kushiriki kwangu ni jambo kubwa na nitahakikisha nafanya vizuri kuisaidia nchi yangu na kuitangaza Simba "amesema.

Banda atakutana na nyota wengine watatu wanaocheza ligi kuu ya NBC ambao ni Prince Dube, Bruce Kangwa, na Never Tigere wa Zimbambwa alio nao kundi moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages