A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, December 1, 2021

RC MAKALLA AITAKA TMDA KUDHIBITI WIZI WA DAWA NA DAWA BANDIA.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla akizungumza wakati wa tukio hilo la mafunzo ya siku tano kwa wakaguzi wa dawa wa Manispaa wa Mkoa wa huo.


- Awataka Kudhibiti wizi wa Dawa za Serikali na kutokomeza Dawa Bandia.

- Asisitiza kufanyika kwa ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kudhibiti wezi wa dawa Na dawa bandia.

- Ataka "vishoka" ambao ni wakaguzi feki kukomeshwa.

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA kupatia ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali na kutoa onyo kwa Maduka yanayonunua dawa za Wizi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Mafunzo ya siku tano kwa Wakaguzi wa Dawa wa Manispaa za Mkoa huo yaliyolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa.

Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeji wa kazi hiyo ambayo inabeba dhamana ya Maisha na uhai wa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka Wanaofanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kubaini wababaishaji na kutaka uwepo wa watoa huduma Wenye sifa na Vigezo.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages