A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, September 13, 2021

YANGA SC YANYUKWA IKIWA NYUMBANI YAKUBALI KIPIGO

 Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV


Young Africans SC sasa itasubiri mchezo wa mkondo wa pili utakaochezwa nchini Nigeria kati ya Septemba 17 na 19, 2021 ili kupata ushindi na kusonga mbele kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United FC, baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 nyumbani katika dimba la Benjamin Mkapa.

Yanga SC wamepoteza mchezo huo uliopigwa leo, 12 Septemba 2021. Huku bao pekee la Rivers United likifungwa na Mchezaji, Moses Omoduemuke katika dakika ya 51 kipindi cha pili, matokeo hayo si rafiki kwa Yanga SC kutokana na Rivers United kupata faida ya bao la ugenini.

Hali ya kukosekana Mashabiki wa Soka katika dimba la Benjamin Mkapa huenda ikawa imewaathiri Yanga SC katika mchezo huo, hali hiyo ya kukosa Mashabiki Uwanjani ni kutokana na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuweka zuio hilo sababu ya janga la UVIKO-19 lililoikumba ulimwenguni.

Yanga SC inakuwa timu ya pili kutoka nchini Tanzania kupoteza mchezo wake wa mkondo wa kwanza hatua za awali wa Michuano hiyo baada ya KMKM SC kutoka visiwani Zanzibar na wao kupoteza kwa bao 2-0 dhidi ya Al Ittihad SC ya Libya kwenye mchezo uliochezwa kwenye dimba la Amani visiwani humo.

Wawakilishi wengine kutoka Tanzania katika Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wataanza ngarambe yao kwenye hatua ya kwanza kati ya Octoba 15 na 17, 2021 dhidi ya Jwaneng Galaxy kutoka Botswana au DFC BEME Arrondssement kutoka Afrika ya Kati, mchezo wa marudiano utachezwa kati ya Oktoba 22 na 24, 2021.


Kiungo wa Yanga SC, Mukoko Tumombe akimiliki mpira mbele ya Wachezaji wa Rivers United FC katika uliochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Yanga SC walipoteza kwa bao 1-0 wakiwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages