A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, September 16, 2021

KMC YATANGAZA KIKOSI CHA WACHEZAJI 29 MSIMU WA LIGI KUU 2021/22

 

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
UONGOZI wa klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) kimetangaza kikosi cha wachezaji 29 kitachoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/22.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC Christina Mwagala imesema kikosi hicho ndicho kitachokuwa kikicheza kwenye msimu wa Ligi Kuu unaotarajia kuanza Septemba 27 mwaka huu.

Benchi la ufundi kwa Msimu wa 2021/22 litasimamiwa na Kocha Mkuu John Simkoko, Kocha Msaidizi ni Habibu Kondo na Hamad Ally, Kocha wa Magolikipa ni Fatuma Omary

Kikosi hicho kimekuwa na maingizo mapya na wengine wakisajiliwa na timu zingine na kwa upande wani Golikipa mkongwe Juma Kaseja na Farouk Shikalo akijiunga na timu hiyo akitokea Yanga, Denis Richard na Sudi Dondola.

Walinzi ni Andrew Vicent Chikupe, Ismail Adam Gambo, Mohamed Kassim, Abdulrazack Mohamed, Kelvin Kijiri, Hassan Khamis Ramadhan, Ally Ramadhan na Nickson Clement Kibabage

Kwa upande wa Eneo la kati, KMC watapata huduma kutoka kwa Jean Baptiste Mugiraneza, Masoud Abdallah Kabaye, Mohamed Samatta, Kenny Ally Mwambungu, Awesu Awesu, Abdul Hillary, Hassan Salum Kabunda, Iddi Kipagwile, Miraji Athuman, Martin Kigi ma Emmanuel Mvuyekure

Washambuliaji ni Matheo Anthony, Sadalla Lipangile, Charles Ilamfia, Nassor Saadun, Hassan Kapalata na Clif Buyoya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages