Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba (kushoto), akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa Benki ya Serikali ya Biashara TCB Kuunganisha huduma za Kibenki Mtandaoni na mifumo ya malipo katika ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw, Sabasaba Moshingi, pamoja na Kaimu Mkugenzi wa Teknolojia na Uwendeshaji wa Benki ya TCB David Nghabi, hafla hiyo imefanyika leo makao kakuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Serikali ya Biashara (TCB)Bw, Sabasaba Moshingi wakati wa uzinduzi rasmi wa Benki ya Serikali ya Biashara TCB Kuunganisha huduma za Kibenki Mtandaoni na mifumo ya malipo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba (kushoto), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Serikali ya Biashara (TCB)Bw, Sabasaba Moshingi alipofika Makao Makuu ya Benki hiyo kwaajili ya Uzinduzi huo.Baadhi ya Maofisa wa Benki ya TCB wakifuatilia hafla na namna gani INTANET inaweza kurahisisha utendaji wa kazi
Meneja
Mwanadamizi Suruhisho za Biashara wa
Benki ya Serikali ya Bishara Leonard Katamba akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
rasmi wa ya TCB Kuunganisha huduma za Kibenki Mtandaoni na mifumo ya
malipo, wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu
wa Serikali, Emmanuel Tutuba ambae ndio alikuwa Mgeni rasmi pamoja na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw, Sabasaba Moshingi
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imekuwa benki ya kwanza
nchini kuunganisha huduma zake za kibenki mtandaoni na mifumo yote ya kitaifa
ya malipo.
Afisa Mtendaji Mkuu wake, Bw, Sabasaba Moshingi, amesema
maboresho yaliyofanyiwa mfumo wa soluhisho hiyo ya kidijitali unaifanya huduma
ya TCB Internet Banking kuwa ya kipekee na isiyokuwa na mpinzani sokoni.
“Suluhisho hii imebuniwa na kutengenezwa na wataalam wetu
wenyewe bila gharama yoyote na ubora wake dhidi ya mifumo mingine ni
kuunganishwa kwake na mifumo yote ya kitaifa ya malipo,” Bw Moshingi
alitabainisha jana wakati wa unzinduzi wake jijini Dar es Salaam.
“Tungeinunua sokoni ingetugharimu kati ya dola 300,000 na
500,000,” alifafanua akionyesha unafuu wake kwani bei hizo ni sawa na TSh
milioni 695.7 na karibu TSh bilioni 1.16 mtawalia.
Kwa mujibu wa Bw. Moshingi, uwekezaji wa kuboresha huduma ni
sehemu ya mpango mkakati wa kuimarisha suhuhishi za kibenki za TCB na kuzifanya
za kisasa zaidi ili ziendane na mahitaji ya soko.
Alisema maboresho ya TCB Internet Banking pia yanalenga
kuiwezesha benki hiyo kujipanga vizuri zaidi kibiashara na kujiimarisha
kiushindani sokoni.
Serikali imeipongeza benki hiyo kwa kufanya maboresho hayo na
kusema yataongeza thamani kwenye mifumo ya kitaifa ya malipo.
Akizumgumza kabla ya kuizindua rasmi huduma hiyo, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw Emmanuel Tutuba, alisema uwekezaji huo
pia unalipa na kuifanya TCB kuwa tishio.
Kiongozi huyo amewahasa wananchi na taasisi zote kujiunga
na mfumo huo mpya wa TCB ili waweze kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi,
usalama na uharaka ili waweze kuongeza ufanisi katika shughuli zao.
“Nimefurahi kusikia kuwa mfumo huu pia umeunganishwa moja
kwa moja na mfumo wa MUSE ili kurahisisha taasisi za serikali kufanya malipo
pasipo na ulazima wa kutembelea benki,” Bw. Tutuba alisema.
MUSE ni mfumo wa ulipaji serikalini ambao ni sehemu ya
mchakato wa serikali mtandao kwa ajili ya kuziwezesha taasisi za umma na
makundi mengine kama watumishi, raia, wanafunzi na wafanyabiashara kupata
taarifa na huduma kwa njia ya intaneti.
Katibu Mkuu Tutuba ameichagiza TCB kutumia umahiri wake wa
ubunifu kusaidia kutafuta ufumbuzi wa maswala mbalimbali na kusaidia kutatau
changamoto mbalimbali kama kupunguza gharama za mikopo na riba kubwa.
Akiutambulisha mfumo huo, Meneja Mkuu Suluhishi
za Biashara wa TCB, Bw Leonard Katamba, alisema huduma hiyo imebuniwa kwa
kuzingatia mahitaji ya sasa na maendeleo ya kidijitali ya siku za usoni.
“Huduma ya TCB Internet Banking itatoa wigo mpana wa huduma
za kibenki kwa wateja wetu; taasisi za serikali, makampuni, mashirika ya dini
na mengine yasiyo ya kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wafanyakazi,
vikundi mbalimbali, taasisi za elimu pamoja na mtu mmoja mmoja,” alifafanua.
“Mfumo huu pia unawazesha wateja kufanya miamala ya kibenki ndani na nje ya nchi kupitia mifumo kama TISS, EFT na SWIFT, ukusanyanji mapato ya serikali na tozo kieletroniki (GePG), miamala ya simu, malipo ya mishahara na kupata taarifa zote muhimu za kibenki.”
MATUKIAO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment