Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa na Viongozi wengine wakiwa katika kikao cha Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi Kinachoendelea ukumbi wa chama wa Jakaya Kikwete Convetion Center Dodoma leo Tarehe 28 April 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na wajumbe wengine wakiwa tayari kuanza kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kinachoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (bara) Ndugu Philip Mangula akisaidiana na Makamu wa Mwenyekiti mwenza (Visiwani) Rais Mstaafu wa Zanzibar Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma leo Jumatano Aprili 28, 2021.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Apiril 28,2021 ameshiriki katika Kikao (Maalum) cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Philip Isdor Mpango, akiwasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichoketi leo jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment