Diwani wa Kata ya Msasani,Kionondoni, Jijini Dar es Salaam,Luca Neghesti, akikagua mifereji anayoijenga kwa nguvu zake binafsi ili kuwaondolea adha ya muda mrefu ya mafuriko wananchi, Dar es Salaam, leo.
WANANCHI wa Kata ya Msasani,Kionondoni, Jijini Dar es
Salaam, wamempongeza Diwani wa Kata hiyo Luca Neghesti kwa jitihada binafsi
anazofanya za kujenga mitaro ya
kupitishia maji ya mvua ili kuwaondolea
adha ya muda mrefu ya mafuriko wakati wa masika.
Wananchi hao walisema kwa miaka mingi kata hiyo ilikuwa
ikikabiliwa na adha kubwa ya mafuriko kutokana na barabara za mitaa kutokuwa na
mifereji hivyo kusababisha adha kwa wananchi.
Wakizungumza leo ,
wananchi hao walisema hatua ya Diwani
Luca kuanza kujenga mifereji hiyo kwa nguvu yake binafsi ni kutambua
haki za wanyonge jambo ambalo
lilitiwa mkazo na Hayati Rais Dk. John Magufuli na kuomba aungwe mkono na
serikali, taasisi, wadau na mashirika
ili kukabiliana na changamoto hiyo.
“Kata ya Msasani tumeteseka kwa miaka mingi na adha ya
mafuriko. Hakuna uongozi uliotukumbuka. Tunamshukuru Diwani Luca ameanza
kuthubutu kutatua kero hii. Kikubwa
tunaomba Halmashauri ya Manisapaa ya Kinondoni , serikali, taasisi wadau na mashirika kumsaidia hata kifusi
tu,”anasema Barnabas Modest Mkazi wa
Mtaa wa Mikoroshini.
Kapilima Ismail, alisema kwa miaka mingi wananchi katika
eneo hilo wamelalamika kuhusu adha kubwa
ya mafuriko kutokana na barabara kuto kuwa na mitaro lakini hawakusikilizwa.
“Diwani Luca tumeanza kuona jitihada zake japo kwa muda
mfupi wa uongozi wake. Tunaamini kama
ataongezewa nguvu basi Kata ya Msasani itarudi katika hadhi yake ,”amesema.
Leila Kibwana aliema,
Diwani Luca anatoa tumaini kubwa kwa wananchi wa kata hiyo ambao mvua
inaponyesha nyumba huzingirwa na maji na katika maeneo mengine maji huingia
ndani na kuleta adha kubwa.
“Tunaomba aungwe mkono hata kwa kifusi.Ameonyesha njia na
mwelekeo kwa kujenga mifereji hii kwa nguvu zake mwenyewe, hii inatokana na
imani kubwa aliyonayo kwetu sisi wananchi wanyonge. Tunaomba wadau wamsaidie kukamilisha kazi hii.
Wananchi hao walise utekelezaji wa Ilani ya CCM si kwa
miradi mikubwa tu bali pia midogo lakini inayo gusa maisha ya wanyonge kama
anavyo tekeleza diwani wao huyo.
Kwa upande wake Diwani Luca (CCM), alisema ameanza ujezi wa mitaro kwa nguvu zake mwenyewe baada
katika mitaa ya Kata hiyo ili kuwanusuru wananchi wake kwa adha ni kubwa
wanayo pata katika kipindi cha
mvua ambapo maji hutapakaa mitaani na hata kuingia ndani ya nyumba.
No comments:
Post a Comment