Meneja Mwandamizi
Kitengo cha Biashara wa Benki ya Biashara ya Akiba Commercial Benki (ACB), David Karosso (kulia), akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za malipo ya Serikali na makusanyo ya kodi zote zinazolipwa
TRA kupitia mfumo wa Kieletroniki
GePG Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo
mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam leo. wengine kushoto Mkuu wa Kitengo cha Kuhamisha Fedha wa Benki hiyo Fredy Chaji, pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa akiba Commercial Benki Dora Saria.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa akiba
Commercial Benki Dora Saria (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa
hafla ya uzinduzi wa huduma za malipo ya
Serikali na makusanyo ya kodi zote zinazolipwa TRA kupitia mfumo wa Kieletroniki
GePG Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo
mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam leo kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara wa Benki ya Biashara ya
Akiba Commercial Benki (ACB), David Karosso pamoja na Mkuu wa Kitengo cha
Kuhamisha Fedha wa Benki hiyo Fredy
Chaji.
Meneja Mwandamizi
Kitengo cha Biashara wa Benki ya Biashara ya Akiba Commercial Benki (ACB), David Karosso (katikati), akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma za Malipo ya Serikali na Makusanyo ya kodi zote zinazolipwa
TRA kupitia mfumo wa Kieletroniki
GePG Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo
mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam leo wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kuhamisha
Fedha wa Benki hiyo Fredy Chaji, na
Meneja Amana za Taasisi wa ACB Fatuma Kigembe. Picha na Brian Peter
Awali ya yote
napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa ajili ya siku njema ya leo. Pia kwa
namna ya pekee napenda kutoa shukarani zangu kwa vyombo vyote vya habari
vilivyojumuika nasi siku ya leo. Karibuni sana.
Akiba Commercial
Bank ni benki ambayo inatoa huduma zake
kwa wateja wa chini na wakati yaani MSME toka kuanzishwa kwake miaka ishirini na
mitatu iliyopita. Benki inatoa huduma zinazolenga na kukidhi mahitaji ya soko
lake. Aidha Benki imekuwa ikifanya tafiti na tathimini za huduma zake mara kwa
mara kwa lengo la kuboresha huduma zake ikiwemo kuanzishwa kwa huduma mpya pale
inapohitajika.
Aidha Benki,
imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 5 ya
azima ya ‘Tanzania ya Viwanda’ kwa kutoa mikopo inayosaidia wajasiriamali mbali
mbali wakiwemo wale wa viwanda vidogo vidogo.
Kama mdau
mmojawapo Benki inaunga mkono jitihada za Serikali za ukusanyaji wa mapato yake
na malipo mbali mbali kwa kuunganisha mifumo ya Benki na Mfumo wa Serikali wa
malipo ya Kielektroniki wa GePG – Government Electronic Payment Gateway.
Matawi yote ya
Benki ya Akiba yanatoa huduma za kukusanya Kodi zote za TRA bila gharama
yeyote. Naomba nisiisitize kuwa huduma
hii ya kufanya malipo ya Serikali
inapatikana kwa watu wote, yaani wateja
wa Akiba na wasiokuwa wateja. Hivyo Walipa kodi wanaweza kujipatia huduma hii
katika matawi yetu yote bila changamoto yeyote, cha msingi ni kuwa na ile
control number ya malipo.
Pia wateja wetu wote
wanaotumia huduma yetu ya Akiba Mobile waweza kufanya miamala ya Malipo mbali
mbali ya Serikali kama kulipia kodi,
Dawasco, Faini za Traffic, Bima za Afya n.k .
Huduma hizi
zinapatika kwa urahisi kabisa na zinaokoa muda na gharama.
Hivyo basi lengo
kuu la kuwaita hapa siku ya leo ni kutoa taarifa rasmi kwa umma wa Tanzania kwa
kuwatangazia kuwa wanaweza kutumia Benki ya Akiba kulipa malipo ya Serikali
zikiwemo kodi zote za TRA na huduma nyinginezo. Aidha, natoa rai pia kwa
taasisi mbali mbali za Serikali kufungua akaunti katika Benki ya Akiba kusudi wananchi
waweze kupata wigo mpana na unafuu zaidi wa kufanya malipo mbalimbali ya
serikali. Hii pia itarahisha na itaboresha mfumo mzima wa ukusanyaji wa mapato
ya
Serikali ambayo
yanasaidia katika shughuli mbali mbali za maendeleo ya wananchi.
Mwisho kabisa,
tunawashukuru wote mlioitikia wito wetu wa kufika na tunaamini kupitia nyie
mtafikisha ujumbe wetu kwa umma na tunategemea mwitikio mkubwa kwa wananchi
kutumia Benki yetu kufanya malipo ya Kodi zote pamoja na malipo mengine ya
serikali. Nia yetu ni kutoa mchango wetu
kwa Serikali katika mchakato mzima wa kuboresha mfumo wa makusanyo wa mapato.
Kwa kumalizia
tunapenda kuipongeza Serikali kwa jitihada zake nzuri za kuboresha mfumo wa
kukusanya mapato kidigitali kwa kuanzisha GePG.
Vile vile
tunaipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania imekuwa
miongoni mwa nchi za Uchumi wa Kati
Tunatoa rai kwa
taasisi zingine za fedha kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukusanya
mapato kwani tunashuhudia mafaniko na
maendeleo ya nchi yetu kupitia nguvu zetu wenyewe.
No comments:
Post a Comment