Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wadau wa sanaa pamoja na waandishi wahabari wakati wa ufunguzi wa msimu wa 11 wa shindano la Bongo star search (BSS) slipway jijini Dar es salaam nakumpongeza madam Ritta kwa kitendo cha uungwana kuomba radhi kwa kuchelewesha kwa malipo ya mshindi wa msimu uliopita Meshack fukuta.
Picha ya pamoja.
Mshindi wa msimu uliopita, Meshack fukuta akitumbuiza baadhi ya nyimbo zinazopatikana katika Ep yake katika hiyo ya ufunguzi wa msimu mpya wa 11 ikiwa imebeba kauli mbiu ya "Mpya kubwa na nusu.
Ritta akiri kuwepo ucheleweshwaji wa malipo
Na Khadija seif, Michuzi tv
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema Madam Ritta kuomba msamaha hadharani ni cha kiungwana sana.
"Mengine sio kwamba uliyasababisha wewe lakini kwa kitendo cha kuomba radhi ni kitendo cha kiungwana Sana nakupongeza."
Pia amemuhakikisha kuwa wizara yake itaendelea kumpa ushirikiano.
"Wizara haiwezi kukuacha kutokana na mchango wako ni mkubwa Sana, na ndio maana nimeweza kuacha ziara na nimeweza kufika kwenye ufunguzi huu wa msimu wa 11."
Aidha,ametoa wito kwa vijana wenyewe vipaji kukimbilia fursa na kuonyesha vipaji vyao.
"Msiache hi fursa ikawapita hivi hivi."
Kwa upande wake Muandaaji wa shindano la BSS, Rita Paulsen amewatoa hofu mashabiki, washiriki na wadau wa shindano la BSS kuwa mwaka huu wameweka mpango mkakati kwa ajili ya kutofanya ucheleweshaji wa zawadi kwa mshindi.
Rita amekiri kuwepo kwa ucheleweshaji wa zawadi kwa msimu uliopita kwa mshindi Meshack na kusababisha sintofaham zilizotokes katika mitandao ya kijamii.
"Nakiri kuwepo kwa ucheleweshaji lakini kwa mwaka huu nawatoa hofu tumejipanga vizuri na tunahaidi kutojirudia tena kwa kadhia hiyo." Amesema Rita
Hata hivyo amewashukuru wadau wanaondelea kuunga mkono jitihada zake za kuhakikisha vijana wanafikia malengo yao hasa kwenye sekta hiyo ya muziki.
"Tukizungumzia BSS tunazungumzia kiwanda ambacho kimeshazalisha waimbaji wengi wakiwemo kala Jeremiah menina, Kayumba, umanne iddi na wengine wengi."
Vile vile amesema BSS inatoa ajira kwa vijana wengi hivyo ni mojawapo ya fursa kubwa kwa vijana wengi.
"Mbali na kutimiza ndoto za vijana wengi kuwa wanamuziki ama waimbaji bali pia imekua ikitoa nafasi kwa watangazaji kama Jokate Mwegelo, Godwin Gondwe,Siza Daniel, Idris sultan pamoja na Vanessa Mdee."
Hata hivyo amewapongeza kampuni ya startimes kwa kuendelea kumpa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha watazamaji wanaendelea Kutumbuiza (kuona show) hiyo kupitia king'amuzi cha startimes kupita chaneli ya startimes Swahili.
"Siku zote nimekua nikifarijika kuona wadau kama startimes wanaunga mkono Jambo langu kwa asilimia kubwa na inanipa Moto wa kuendelea kuhakikisha nasongesha gurudumu hili la kusaka vipaji kutokana na uwepo wao."
Pia ametaja mikoa mitano ambayo watafika kwa ajili ya kuanza rasmi mchakato wa kusaka washiriki kwa msimu wa 11.
"Tunatarajia kuzunguka katika mikoa mitano kuanzia septemba 19 Mbeya, Arusha, Mwanza Dodoma pamoja na Dar es salaam na kwa mara ya Kwanza tumekuja na kauli mbiu ya "Mpya kubwa na nusu."
No comments:
Post a Comment