A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, August 20, 2020

BENKI YA NCBA YAAPA KUSAIDIA UKUAJI WA BIASHARA ZA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI NCHINI TANZANIA

 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dokta Ashatu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi benki mpya ya NCBA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume na Mwenyekiti wa bodi ya NCBA, Sharmapal Aggarwal.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dokta Ashatu Kijaji akizungumza na wafanyakazi wa Benki mpya ya NCBA na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Limited, Margaret Karume akizungumza na wafanyakazi wa Benki mpya ya NCBA na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NCBA wakiongozwa na bendi ya polisi kwenye maandamano ya sherehe za uzinduzi wa benki ya NCBA jijini Dar es Salaam.
  • Benki yaelezea namna itakavyokuwa mstari wa mbele kuleta uwezeshaji wa kiuchumi kupitia ujumusishwaji wa kifedha huku ikiwahamasisha wanaojituma kufikia malengo yao ya ukuaji 
Agosit 19, 2020 - Benki ya NCBA yaapa kusaidia biashara za viwanda vidogo na vya kati ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya NCBA Margaret Karume kwenye kusheherekea ujio wa Benki hio nchini, tukio likiambatana na uzinduzi wa Makao Makuu ya Ofisi ya NCBA na Tawi lao Kuu mtaa wa Ohio, Amani House jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Margaret Karume alisema kuwa, malengo ya Benki ni kuhamasisha wanaojituma kwenye safari yao ya mafanikio na kuchochea ukuaji wa kiuchumi nchini na zaidi. ‘Kupitia uvumbuzi wetu unaomzingatia mteja na uwekezaji kwenye bidhaa za kidijitali za benki, tuko tayari kuharakisha ukuaji na maendeleo katika sekta muhimu za kiuchumi kama vile biashara za viwanda vidogo, vya kati, mashirika, miradi mikubwa ya miundombinu na sekta ya kilimo’.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages