Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kwamba atatuma maafisa wa kijeshi kwenye miji ya Chicago na Albuquerque katika jimbo la New Mexico kusaidia kukabiliana na ongezeko la matukio ya kihalifu, hatua inayozidisha uingiliaji kati wa serikali kuu kwenye serikali za majimbo katika kipindi ambacho anawania kurejea tena madarakani akitumia kauli mbiu ya amani na sheria.
Wataalamu wa masuala ya sheria za jinai wanasema, hata hivyo, maelezo haya ya Trump kuhusiana na ongezeko la uhalifu hayana mashiko. Wanasema uamuziwake huo ni mbinu ya kujijenga kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa Novemba, hasa baada ya kadhia ya virusi vya korona kuathiri pakubwa mtazamo wa wapigakura kumhusu rais huyo
No comments:
Post a Comment