Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli Mpya ya Kisasa ya Standard gauge kwaajili ya Usafiri wa Treni Umeme inayoanzia Dar es salaam hadi Makutupora Dodoma na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa mapinduzi makubwa kwenye usafiri wa Reli.
Akiwa kwenye Ujenzi wa Jengo la Abiria ambalo ujenzi wake umefikia 80%, RC Makonda amewataka Wafanyabiashara kuanza kuchangamkia fursa ya kufungua Biashara mbalimbali kwenye Jengo hilo la Gorofa nne ikiwemo Supermarket, Maduka, Migahawa, Mall's na huduma za kifedha ikiwemo Bank na Mitandao ya Simu.
Aidha RC Makonda amesema kwa sasa Serikali ipo kwenye hatua ya kuanza ujenzi wa Reli kwaajili ya Treni ya katikati ya mji ikianzia Kerege Bagamoyo hadi maeneo ya mjini ikiwemo posta kwa lengo la kurahisisha shughuli za usafiri.
Kwa Mujibu wa Shirika la Reli Tanzania TRC ujenzi wa Reli kutoka Dar es salaam, Morogoro hadi Dodoma Makutupora unagharimu zaidi ya Shilingi Trillion 7.2.
No comments:
Post a Comment