A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, July 30, 2020

Rais Magufuli amewasisitiza Watanzania kuendelee kumwombea Mkapa


Na Faruku Ngonyani , Mtwara



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewataka watanzania waendelee kumuombea Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa taifa hilo Benjamin William Mkapa na kuwasisitiza kuiga tabia zote njema alizokuwa nazo wakati wa uhai wake ikiwa pamoja kuwa mzalendo wa kweli na kupenda nyumbani kwao.



Rais Magufuli amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye mazishi ya Hayati Benjamin Mkapa yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia kijijini kwao Lupaso, wilayani Masasi Mkoani Mtwara.



Magufuli amesema Mkapa aliyaishi maisha yenye upendo wa kweli na alipenda nyumbani kwao kwani hata pale serikali ilivyojaribu kutenga eneo maalumu la kuzikia viongozi wa kitaifa jijini Dodoma alipinga wazo hilo na kuagiza atakapofariki azikwe kijijini kwao kwenye makaburi ya familia.



Awali kabla ya kutoa salamu Rais Magufuli alipokea salamu za rambirambi kutoka ubalozi wa makao makuu ya kanisa Katoliki, Vatican, taifa la Msumbiji na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.



Aidha Kwa upande wake Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho kikwete amemuelezea Hayati Benjamin Mkapa kama kiongozi aliyechukia nchi na watu wake kuwa umaskini na kulipa kipaumbele suala la uchumi na kupelekea kuanzisha dira ya taifa ya kufikia uchumi wa kati ifakapo mwaka 2025 na pato la mtanzania mmoja kufikia dola 3000.



Ameongeza kuwa  Hayati Benjamin Mkapa alikuwa kiongozi mwenye utambuzi na manufaa kwa wananchi wake kwa kuwa alipenda kusikiliza, kushughulikia changamoto na kutoa mrejesho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages